JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TANZANIA NA BELARUS ZASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KUHSIRIKIANA NYANJA YA UCHUMI

Share This

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika Uchumi, mkataba huo umesainiwa leo Aprili 29, 2026 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov wakionesha mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika Uchumi, mkataba huo ambao wameusaini leo Aprili 29, 2026 jijini Dar es Salaam.


SERIKALI ya Tanzania na Belarus zimesaini mkataba wa makubaliano (MoU) ya kuanzisha kamati maalumu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, hatua inayolenga kuratibu mahusiano yao na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Aprili 29 2026 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov.

Akizungumza baada ya kusaini ushirikiano huo, Profesa Kitila anasema hatua hiyo inalenga kufufua mahusiano kati ya Tanzania na Belarus ambayo yanasimama kwa takribani miaka 30 iliyopita.

Amesisitiza kuwa makubaliano hayo yanafungua fursa za uwekezaji kutoka Belarus katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, viwanda na biashara, hali inayotarajiwa kuongeza ajira na mapato ya taifa.

Aidha, amesema ushirikiano huo utaisaidia Tanzania katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050 kwa kuvutia wawekezaji wapya, kuleta teknolojia za kisasa na kuongeza ushindani wa uchumi.

Katika hatua nyingine, Profesa Mkumbo amebainisha kuwa kuna mpango wa kupeleka vijana nchini Belarus ili kujifunza teknolojia mbalimbali, hususani zitakazosaidia kuboresha sekta ya kilimo.

Kwa upande wake, Ryzhenkov amesema anafuraha sana kwamba wamesaini makubaliano ya kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Biashara na Uchumi na hicho kitakuwa chombo muhimu kwa mahusiano yao.

Amesema wanaitazama Tanzania kama mshirika muhimu na lango lao kuu la ukuaji katika ukanda huu, hivyo wapo tayari kuwekeza katika miradi ambayo haitachochea tu biashara kati ya nchi zao, bali pia kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kimkakati kwa biashara yetu barani Afrika.

“Tunaitazama Tanzania kama mshirika muhimu na lango letu kuu la ukuaji katika ukanda huu. Tuko tayari kuwekeza katika miradi itakayoiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha kimkakati cha biashara barani Afrika,”amesema Ryzhenkov.

Amesema katika ziara yao, walitembelea maeneo kadhaa ya kuvutia, ikiwemo maeneo ya usindikaji wa bidhaa za mauzo ya nje na kwa sasa wanatafakari namna bora ya kushiriki kikamilifu katika mifumo hiyo.

Pia amesema kampuni kadhaa za Belarus zimeonyesha nia ya kutumia maeneo hayo hususani kuna nia ya kuanzisha kituo cha kikanda cha mbolea na bidhaa nyingine kitakachohudumia si Tanzania pekee bali pia ukanda mpana wa Afrika Mashariki.

Ryzhenkov amesema makubaliano mengine kadhaa ya msingi yako mezani kwa sasa lakini hadi kufikia ziara ya Waziri Mkuu wao Oktoba, mwaka huu watakuw awamekamilisha, makubaliano hayo yakiwemo ulizi wa uwekezaji na ushirikia no katika huduma za forodha.

Amesema mbali na biashara anatarajia kuona ushirikiano wao ukitanuka hadi kwenye masuala ya kibinadamu, mazungumzo ya kisiasa na mambo ya nje, yeye na wenzake na wamejizatiti kurahisisha mahusiano hayo na kuimarisha ushirikiano wa biashara kwa biashara pamoja na watu kwa watu

Pia amesema wako tayari kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vyuo vikuu vya nchi zote na vituo vya utafiti ili kukuza miradi ya pamoja ya utafiti yenye manufaa kwa pande zote na kuleta karibu zaidi jumuiya za kisayansi za nchi zao.








Matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad