▪︎ Aagiza mradi ukamilike kwa wakati na ubora, asisitiza malipo kwa wafanyakazi wa mradi yafanyike kwa wakati
▪︎Awapongeza watumishi wa afya kwa weledi
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mradi wa ujenzi wa jengo la huduma (Wing B) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi lazima ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Akizungumza leo Jumatatu 16 Machi, 2026 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo katika hospitali hiyo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Waziri Mkuu amesema Serikali imehakikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Akizungumza leo Jumatatu 16 Machi, 2026 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo katika hospitali hiyo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Waziri Mkuu amesema Serikali imehakikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.“Matarajio yetu ni kuona mradi unakamilika kwa wakati na kuwa na ubora unaotakiwa. Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya mradi huu, hivyo sitarajii kuona kuna madeni kwa watu waliofanya kazi katika mradi huu,” amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma.
Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma.“Ninyi mnaofanya kazi nzuri msiingiwe na ubaridi kwa sababu Serikali inaendelea kuwachukulia hatua wale wote wanaobainika kufanya uzembe kazini. Bila ninyi watendaji mnaofanya kazi kwa bidii na weledi, nchi yetu isingekuwa na maendeleo tunayoyaona leo,” amesema.
Kadhalika, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watumishi bora katika sekta ya afya katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), huku akisisitiza kuwa watumishi watakaobainika kufanya uzembe kazini watachukuliwa hatua stahiki.
Kadhalika, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watumishi bora katika sekta ya afya katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), huku akisisitiza kuwa watumishi watakaobainika kufanya uzembe kazini watachukuliwa hatua stahiki.Aidha, Waziri Mkuu amesema kwa takribani miaka 60 baada ya uhuru, wilaya zote za Mkoa wa Katavi hazikuwa na hospitali za wilaya. Amesema mafanikio ya ujenzi wa hospitali mbalimbali yamepatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Deogratias Banuba, amesema ujenzi wa jengo la huduma (Wing B) unagharimu takribani shilingi bilioni 13.28 na hadi sasa umefikia asilimia 59 ya utekelezaji.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Deogratias Banuba, amesema ujenzi wa jengo la huduma (Wing B) unagharimu takribani shilingi bilioni 13.28 na hadi sasa umefikia asilimia 59 ya utekelezaji.Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Februari 14, 2023 na unatarajiwa kukamilika Desemba 13, 2026. Kukamilika kwa jengo hilo kutaiwezesha hospitali hiyo kuwa na wodi za kujifungulia, vyumba vya upasuaji pamoja na wodi ya kulaza watoto, ambazo kwa sasa hazipo.
Kwa sasa hospitali hiyo ina watumishi 475 sawa na asilimia 61.5 ya mahitaji, huku ikiwa na madaktari bingwa 13 katika fani mbalimbali na lengo ni kufikia madaktari bingwa 17 ifikapo mwaka 2030.
Kwa mujibu wa Dkt. Banuba, huduma za kibingwa zinazotolewa katika hospitali hiyo ni pamoja na afya ya uzazi na mtoto, upasuaji, mifupa na ajali, masikio pua na koo, ganzi (Anesthesia), afya ya akili, macho, radiolojia pamoja na huduma ya uchujaji wa damu (Dialysis).
Kwa mujibu wa Dkt. Banuba, huduma za kibingwa zinazotolewa katika hospitali hiyo ni pamoja na afya ya uzazi na mtoto, upasuaji, mifupa na ajali, masikio pua na koo, ganzi (Anesthesia), afya ya akili, macho, radiolojia pamoja na huduma ya uchujaji wa damu (Dialysis).Katika hatua nyingine, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Tasker Mbogo, aliwasilisha ombi kwa Waziri Mkuu akiomba Serikali ijenge eneo la kusubiria wagonjwa (waiting bay), chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na uzio wa hospitali hiyo.
Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Reuben Kwagila, amesema Serikali imepanga kupeleka takribani shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuongezea majengo ya wodi, ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na ujenzi wa uzio wa hospitali hiyo.
Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi na maeneo ya jirani, hususan huduma za mama na mtoto pamoja na huduma za kibingwa.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha mradi huo unasimamiwa ipasavyo ili ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.


No comments:
Post a Comment