*Kuzindua kitabu cha "Quick Guide kwa ajili ya kutoa mongozo kuhusu huduma ya kwanza
*Kuwakutanisha wadau sekta ya anga Aprili 4,pia kuweka kambi uchunguzi wa afya
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIKA kuadhimisha miaka mitano ya taasisi ya Aerospace Medical and Training Centre(AMTC) inatarajia kufanya hafla maalum itakayohusisha wadau pamoja na maonesho ya maendeleo ya afya ya sekta ya anga katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.
Wakati wa maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Aprili 4,2026 pia kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa kitabu cha "Quick Guide to ambacho kitatoa mongozo mfupi na wa vitendo kuhusu huduma ya kwanza katika sekta ya anga, kilichoandalia kwa ajili ya wahudumu wa ndege, watanyakazi wa ardhini, wanatunzi wa marunzo ya anga pamoja na wadau wa sekta ya usafiri wa anga.
Kitabu hicho kitapatikana kidijitali kupitia Amazon na Kindle pamoja na majukwaa mengine ili maarifa haya yaweze kuwafikia wataalamu duniani kote.
Akizungumza leo Machi 16,2026 jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji Aerospace Medical and Training Centre Dk. Nasra Nassor Omar amesema pia wakati wa maadhimisho hayo kutafanyika uzinduzi wa mfumo wa mafunzo na mitihani mtandaoni wa AMTC (Online Training Centre).
Amefafanua mfumo huo utatoa fursa kwa wataalamu wa sekta ya anga kupata maunzo ya tiba ya anga, kufanya mitihani na kupata vyeti kupitia simu au kompyuta bila ya kuhitaji kusafiri. “Hii ni hatua muhimu katika kupanua upatikanaji wa mafunzo ya kitaalamu chini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia amesema kutakuwa na kampeni ya chunguzi wa afya kwa wafanyakazi wa sekta ya anga huku akifafanua kwa kutambua kuwa afya bora ni msingi wa usalama wa kazi, AMTC itaendesha zoe la uchunguzi wa afya katika Viwanja vukuu vya ndege
“Machi 31 Machi 2026, uchunguzi utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, ambapo takribani wafanyakazi 200 wa sekta ya anga watapatia huduma za uchunguzi wa afya.
“Kisha Aprili 1 hadi 2 Aprili 2026, uchunguzi wa afya utaendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam (Terminal 1 na 2) ambapo zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya anga watashiriki katika chunguzi wa afya na mafunzo ya uhamasishaji wa afya.
“Vipimo vitakavyotolewa vitajumuisha uchunguzi washinikizo la damu, sukari katika damu, malaria, kiwango cha damu mwilini, pamoja na hamasishaji na uchunguzi wa awali wa saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti, na saratani ya tezi dume.”
Dk.Nasra Omar amesema hatua hizo zinaweza kusaidia kugundua changamoto za kiafya mapema na kulinda afya ya wafanyakazi wa sekta ya anga.Dhamira yao katika AMTC inaendelea kuwa moja kuhakikisha kila mtaalamu wa sekta ya anga anakuwa na mafunzo sahihi, afya bora na uwezo wa kukabiliana na dharura, ili kulinda usalama wa abiria na wafanyakazi wote wa sekta hii.
Akieleza zaidi amesema miaka mitano iliyopita walianza kwa sababu waliona hitaji na leo wanaona matokeo huku akisisitiza na safari yao bado inaendelea.
“Tunawaalika wadau wote wa sekta ya anga, mashirika ya ndege, waendeshaji wa viwanja vya ndege, mamlaka za udhibiti, washirika wa sekta ya afya pamoja na vyombo vya habari kushiriki nasi katika hatua hii muhimu.Kwa pamoja tunaweza kuendelea kuimarisha afya na
usalama wa sekta ya usafiri wa anga chini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.”
Kuhusu taasisi ya AMTC) ambayo mwaka huu inaadhimisha miaka mitano tangu ilipoanzishwa imejikita katika uchunguzi wa afya kwa wataalamu wa anga kabla ya kupata leseni za kuruka,mafunzo ya tiba ya anga, maandalizi ya huduma za tiba ya dharura (First Aid), pamoja na kuimarisha afya na ustawi wa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga nchini Tanzania
“Hebu fikiria hali ambapo abiria anapata mshtuko wa moyo ndani ya ndege akiwa futi 35,000 juu angani.Katika wakati huo, maisha yake yanategemea uwepo wa mhudumu wa ndege au mtaalamu aliyepata mafunzo sahihi ya huduma ya kwanza na fufuaji wa mapigo ya moyo na mapafu (CPR), au hata uwepo wa daktari mwenye ujuzi huo ndani ya ndege.
“Maarifa haya yanaweza kuleta tofauti kubwa kati ya uhai na kifo.Hii ndiyo sababu kuu iliyotusukuma kuanzisha AMTC kuhakikisha kuwa wataalamu wa sekta ya anga wanakuwa na mafunzo sahihi, maandalizi ya kitabibu na uelewa wa kukabiliana na dharura, ili kulinda usalama wa abiria, wafanyakazi wenzao na jamii kwa ujumla.”






No comments:
Post a Comment