JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Valentine’s Day Yaja na Msisimko Mpya: Mati Super Brands Ltd Yazindua 'Royal Love Challenge 2026'

Share This

 

 

Dar es Salaam — Kampuni ya Mati Super Brands Ltd kupitia kinywaji chake cha kifahari cha Tanzanite Royal Gin imezindua rasmi kampeni maalum ya msimu wa Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ijulikanayo kama “Tanzanite Royal Gin – Royal Love Challenge 2026”, yenye lengo la kuimarisha uhusiano na wateja pamoja na kusherehekea mapenzi kwa njia ya kipekee.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Izack Piganio, Meneja wa Chapa Mati Super Brands, alisema, "Royal Love Challenge ni njia yetu ya kuwapa wateja uzoefu wa kipekee wa kusherehekea Valentine’s Day, huku tukijenga uhusiano wa karibu na wapenzi na wanandoa kupitia chapa ya Tanzanite Royal Gin. Tunataka mapenzi yashehereke kwa hadhi ya kifalme, na washiriki washindwe kwa ubunifu na upendo wao."
Shindano hili la mtandaoni litafanyika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, likiwalenga wapenzi, couples na wanandoa. Washiriki wanatakiwa kupiga picha wakionyesha upendo wao pamoja na chupa halisi ya Tanzanite Royal Gin, kisha kuipakia kwenye akaunti zao za Instagram. Ili kushiriki kikamilifu, washiriki wanapaswa kutag ukurasa rasmi wa @TanzaniteRoyalGin, kutumia hashtag #RoyalLoveChallenge, na kufanya collaboration na ukurasa wa kampeni.

Kwa upande wake, Meneja wa hoteli ya Asmorain, Amina Mrutu, alisema: "Tunakufariji kuwa sehemu ya kampeni hii ya Royal Love Challenge. Tunatarajia mshindi atapata zawadi za kipekee zenye mchanganyiko wa mapenzi na burudani, ikiwemo usiku mmoja katika hoteli yetu, chakula cha jioni cha kimapenzi na safari ya kupumzika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire."

Mshindi wa Royal Love Challenge 2026 atatangazwa Februari 12, 2026, huku zawadi zote zikitolewa rasmi Februari 14, siku ya Valentine’s Day. Kampeni hii inatarajiwa kuleta burudani, ushindani chanya, na kuendeleza utamaduni wa kusherehekea mapenzi kwa hadhi ya kifalme.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad