TAASISI inayohusika na Elimu ya Juu Afrika Mashariki(IUCEA)imevutiwa na uwekezaji unaofanywa na Serikali ya Tanzania kuhusu ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi nchini kwani programu zinazoendeshwa na vyuo hivyo zinatoa fursa za ajira kwa vijana wa ukanda huo.
Viongozi mbalimbali kutoka vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wanaounda umoja huo wametembelea chuo cha VETA Mkoa wa Kagera kwa lengo la kujionea program mbalimbali za ufanisi dinazotoa fursa kwa vijana kujajiri katika nchi yeyote pamoja na kusajiliwa
Akizungumza Katibu wa Umoja wa IUCEA Profesa Maw Michael amesema kwa miaka ya nyuma umoja huo ulikuwa ukjihusisha na vyuo vikuu lakini miaka nane iliyopita huku akifafanua umoja huo ulianza kujihisisha na vyuo vya Ufundi stadi.
Amesema kuwa lengo la kuhamasisha vijana wa Africa Mashariki kubadilishana uzoefu katika fani mbalimbali na kujaribu kuweka sera za kielimu zinazofanana ili kurahisisha upatikanaji ajira katika mipaka yote Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Tanzania, Dkt. Abdallah Ngodu, amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha vijana wasiopungua 120,000 wanahitimu mafunzo ya ufundi stadi kila mwaka ili kuimarisha nguvu kazi ya taifa.
Amesema katika mwaka uliopita, jumla ya vijana 86,000 walihitimu kutoka vyuo mbalimbali vya VETA nchini, hatua inayodhihirisha ukuaji mkubwa wa sekta ya elimu ya ufundi stadi.
“Hadi sasa nchini kuna takribani vyuo 80 vya VETA vinavyotoa mafunzo, huku vyuo vingine 65 vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.Lengo la ziara ya washirika hao ni kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Tanzania katika sekta ya elimu ya ufundi stadi pamoja na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kukuza ujuzi kwa vijana wa Afrika Mashariki.
Aidha amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha elimu ya ufundi stadi inawafikia wananchi wote bila ubaguzi.VETA inatoa nafasi kwa jinsia zote pamoja na makundi maalumu ili kila Mtanzania aweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi,” alisema Ngodu.
Wakati huo huo Mratibu wa Kanda ya Afrika, Dkt. Cosma Chawana Joseph, amesema kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimeongeza uwekezaji katika sekta ya ufundi stadi kwa kuwa ndiyo njia kuu ya kujenga ujuzi, maarifa mapya na nguvu kazi ya vijana.
Pia amesema ziara yao katika Chuo cha VETA Kagera imewapa fursa ya kujionea kwa vitendo Tanzania ilivyowekeza kwa kiwango kikubwa katika vyuo vya ufundi stadi, hasa vyuo vikubwa vya VETA.
“Nchi za Afrika zinaendelea kushirikiana kuboresha elimu ya ufundi stadi. Hakuna ushindani, bali tunalenga kudumisha ushirikiano imara kwa maendeleo ya pamoja ya bara letu.”







No comments:
Post a Comment