JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

NEC YAWAFUNDA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WA SAIDIZI WA VITUO VYA KURA JIMBO LA PERAMIHO

Share This
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 23, 2026 ametembelea mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma na kuzungumza nao ambapo amewasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kufuata Sheria, Kanuni na maelekezo ya Tume.

Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika katika Kumbi tatu tofauti za Seminari Kuu Peramiho, Maposeni Sekondari na Ukumbi wa Josephat Mkuwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Peramiho ambao unatarajiwa kufanyika Februari 26, 2026 na utashirikisha vyama vya siasa 15.

Wajumbe wengine wa Tume walitembelea vituo hivyo vya mafunzo na kuzungumza na washiriki hao. 

Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wakisikiliza nasaha za viongozi wa Uchaguzi walipotembelewa katika kituo cha mafunzo kilichopo Ukumbi wa Seminari Kuu Peramiho.  
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka INEC ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza jambo. 
Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wakisikiliza nasaha za viongozi wa Uchaguzi walipotembelewa katika kituo cha mafunzo kilichopo Ukumbi wa Seminari Kuu Peramiho. 
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Peramiho, wilayani Songea mkoani Ruvuma Ndg. Exavery Luyagaza akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo kituo cha Seminari Kuu Peramiho.

Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wakisikiliza nasaha za viongozi wa Uchaguzi walipotembelewa katika kituo cha mafunzo kilichopo Ukumbi wa Seminari Kuu Peramiho. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri, leo Februari 23, 2026 ametembelea na kukagua Mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupiga Kura katika jimbo la Peramiho, Songea mkoani Ruvuma. 

Mjumbe huyo wa Tume amewapongeza washiriki wa mafunzo na kuwataka kuzingatia weledi na kuwakumbusha kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha matatizo kama yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Balozi Mapuri amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuwa mafanikio ya uchaguzi yatatokana na wao kuzingatia mafunzo waliyoyapata ili kufanikisha uchaguzi huu mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 26, 2026 kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama.

Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma waliokua katika kituo cha mafunzo cha Maposeni Sekondari wakisikiliza nasaha za viongozi wa Uchaguzi. 
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 23 Februari, 2026 ametembelea na kukagua mafunzo kwa makarani wasimamizi na wasimamizi wasaudizi wa vituo vya kupugia kura yaliyofanyika katika ukumbi wa Josephat Mkuwa uliyopo halmashauri ya wilaya Songea Mkoani Ruvuma ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Peramiho utakaofanyika siku ya Alhamisi tarehe 26 Februari, 2026.

Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma waliokua katika kituo cha mafunzo cha Josephat Mokuwa wakisikiliza nasaha za viongozi wa Uchaguzi. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad