JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MENEJIMENTI YA TMDA YAJIPANGA NA DIRA 2050

Share This

Menejimenti ya TMDA yakutana Morogoro tarehe 2 -3 Februari, 2026 kujadili rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Mamlaka wa miaka mitano, 2026/27-2030/31 unaoakisi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050. 

Rasimu ya Mpango Mkakati huo ni ya Sita kufuatia kukamilika kwa ufanisi kwa Mpango Mkakati wa Tano. Mpango Mkakati wa Sita wa TMDA unatarajiwa kuanza kutumika mnamo tarehe 01, Julai, 2026.

Pamoja na mambo mengine, rasimu ya Mpango Mkakati husika inalenga katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kulinda afya ya Jamii. 

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, aliwaeleza wajumbe wa kikao husika kuwa rasimu husika ya Mpango Mkakati inabeba Dira mpya ya TMDA ambayo ni "Kuimarika kwa afya na ustawi wa Watanzania wote kupitia udhibiti bora unaokidhi viwango vya kitaifa". 

Dkt. Fimbo aliongeza kuwa,  Dhamira Mpya ya Taasisi itakuwa " Kulinda  Afya ya Jamii kwa kuhakikisha, usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa zote zinazohusiana na afya".

Uongozi wa TMDA imekuwa na utamaduni shirikishi katika kujadili mambo makubwa yahusuyo taasisi, ambapo watumishi wote hushirikishwa kupitia ngazi mbalimbali ndani ya Mamlaka kabla ya kuidhinishwa na Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB).

Pamoja na mambo mengine, Mpango Mkakati huu mpya unaweka mwelekeo wa pamoja katika udhibiti, utasaidia katika kupanga matumizi ya rasilimali vizuri na kuboresha uwajibikaji na uwazi.

Mpango Mkakati wa TMDA ni nyaraka muhimu ambayo inaonesha ramani ya safari ya taasisi na ndiyo chombo muhimu cha kuongoza maamuzi na maendeleo ya TMDA.
Mkurugenzi Mkuu TMDA, Dkt. Adam Fimbo, akifafanua jambo katika kikao cha Wakurugenzi na Mameneja

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Adam Fimbo na Bw. Chrispin Severe, Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma katika kikao cha Wakurugenzi na Mameneja.

Dkt. Kissa Mwamwitwa, Mkurugenzi Udhibiti Vifaa tiba na Vitendanishi, akichangia hoja katika kikao.

Sehemu ya Mameneja wakifuatilia kikao

Mkurugenzi  wa Udhibiti wa dawa za binadamu na mifugo, Dkt. Yonah Mwalwisi, akichangia jambo katika kikao

Bi. Gaudensia Simwanza, Meneja Mawasiliano na Elumu kwa Umma, akichangia hoja katika kikao



Wataalam wa Mipango na Tathmin wakijadili jambo wakati wa kikao





 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad