MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila mapema leo amefika eneo la mgogoro wa nyumba ya Mama mjane Block D Kunduchi Wilaya ya Kinondoni ambapo ameagiza kuundwa kamati maalumu chini ya ofisi yake huku pia akimueleleza mkuu wa wilaya ya kinondoni Mhe Saad Mtambule kuunda kamati nyingime ili kamati hizo ziweze kushughulikia kwa haraka mgogoro huo na haki ipatikane kwa wakati.
Mgogoro huo unahusisha nyumba pamoja na viwanja namba 38,39 na 40 blok D vilivyoko kunduchi beach Kinondoni, ukimhusisha Happiness Mwambingu ambae ni mjane wa marehemu Dkt Benard Mwambingu na Fots Mwambingu ambae ni mdogo wa marehemu alieamua kubadilisha hati ili kujimilikisha nyumba na viwanja vya aliekuwa kaka yake.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo na kusikiliza namna mgogoro huo ulivyo, pamoja na uamuzi wa kuunda kamati hizo mbili RC Chalamila ameliamuru Jeshi la polisi kumkamata Lidia Benard na Joel Mwambingu ambao walifanya udanganyifu ili kujimilikisha eneo hilo na hatimaye likauzwa ambapo Lidia Benard alijifanya ni mke wa marehemu huku Joel akijifanya ni Mtoto wa Marehemu.
Aidha kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema kwa kuwa kumekuwa na sintofahami nyingi kwenye viwanja na nyumba hiyo hadi kuuzwa na kwamba mjane huyo alipaswa kuondoka kwenye nyuma hiyo ameelekeza mjane huyo kuendelea kuishi hapo hadi pale watakapojiridhisha juu ya mmiliki halali
Sanjali na hilo Mjane wa marehemu Bi Happiness na Mwanasheria wa kamishna wa ardhi Adelifrida Lekule wameeleza hali halisi ya mgogoro huo ulivyo hadi kufikia hapo ulipo ambapo nyumba hiyo tayari imeuzwa na mjane huyo kutakiwa kuondoka kwenye nyumba hiyo.
Mwisho moja ya mambo yanayoleta utata ni kijana Joel kuwa yeye ni mmiliki wa nyumba na viwanja hivyo tokea miaka ya 1980 wakati yeye mwenyewe amezaliwa mwaka 1996
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


No comments:
Post a Comment