Dar es Salaam- Desemba 15, 2025
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho, amesema hayo leo wakati akifungua rasmi mafunzo elekezi kwa watumishi wapya 60 wa kada mbalimbali walioajiriwa hivi karibuni na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika kampasi sita za Dar es Salaam, Mtwara, Singida, Tabora, Tanga na Mbeya.
Dkt. Mabonesho amesisitiza kuwa, uendeshaji wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya ni wa lazima kwa kuzingatia utekelezaji wa Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 05 wa mwaka 2022, unaowataka kila mwajiri kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wapya wanapatiwa mafunzo mara wanapoanza kazi.Pia ameeleza kuwa, mafunzo elekezi yanakusudia kuwapa watumishi uelewa wa pamoja kuhusu Sheria, Kanuni, Taratibu na Maadili katika Utumishi wa Umma.
Aidha, Dkt. Mabonesho ameongeza kuwa, Chuo cha Utumishi wa Umma ni kitovu cha ubora wa utoaji huduma kwautumishi wa umma nchini,hivyo, watumishi wapya wana mchango katika kuboresha huduma zinazotolewa, ikiwemo mafunzo, ushauri, na utafiti.
“Kila mtumishi anapaswa kuwajibika, bidii ya kazi, moyo wa kujifunza, kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia taratibu, kanuni na sheria katika utendaji kazi” amesema Dkt. Mabonesho.
Amesisitiza kuwa, watumishi wapya wanatakiwa kuzingatia mafunzo hayo kwa kuwa yatawaongezea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



No comments:
Post a Comment