JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Dar City, Fox Divas watwaa ubingwa wa betPawa NBL 2025

Share This

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Timu ya Dar City kwa upande wa wanaume na Fox Divas kwa upande wa wanawake zimetwaa ubingwa wa mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2025) yaliyomalizika Jumamosi kwenye uwanja wa Chinangali, mkoani Dodoma.

Dar City ilitwaa kombe hilo baada ya kuichakaza Kisasa Heroes kwa pointi 80-51 wakati Fox Divas iliisambaratisha timu ya Vijana Queens kwa pointi 65-57.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa timu za Dar City na Fox Divas kutwaa Ubingwa wa ligi ya betPawa NBL. 

Kwa mujibu wa rekodi za mashindano hayo, Dar City na Fox Divas kila mmoja zimejizolea zawadi nono kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) ya betPawa ambapo kila timu imejishindia Sh20.1 milioni kwa kushinda mechi zote za mashindano hayo.

Timu zilizofuatia kulipwa fedha nyingi kupitia LRB ni Dodoma Spurs na JKT kwa upande wa wanaume ambapo kila moja ilishinda Sh15.6 milioni  huku timu za Kisasa Heroes na Vijana Queens zilishinda kiasi cha Sh13.4 milioni kila moja.

Timu za wanawake za JKT Stars na DB Lioness kila moja ilipata Sh11.2 milioni..

Fedha hizo zililipwa moja kwa moja kwa Wachezaji na makocha kupitia simu zao za mikononi. Lengo ni kuwanufaisha na kutambua bidii zao kwa kushinda mechi.

Mbali ya kuzoa fedha nyingi katika LRB, Dar City na Fox Divas walizawadiwa  pia Sh 2.5 millioni  kila moja kutoka betPawa kwa kuwa washindi wa jumla.

Washindi wa pili wa mashindano hayo walizawadiwa Sh1.5 millioni  na timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu, zilizawadiwa Sh500,000.

Timu ya Bright Queens ya Dodoma ilishinda zawadi ya timu yenye nidhamu kwa upande wa wanawake wakati kwa wanaume timu ya Manyara ilishinda zawadi hiyo.

Katika zawadi za mchezaji mmoja mmoja, Evelyne Nakilingi wa Fox Divas alishinda tuzo ya mchezaji bora na kuzawadiwa Sh500, 000 ambapo kwa wavulana zawadi hiyo ilikwenda kwa  Romis Bujeje wa Kisasa Heroes.

Pia Ekone Brenda wa Fox Divas alishinda zawadi ya mfungaji bora huku zawadi ya beki bora ilikwenda kwa Taudensia Katumbi wa DB Lioness na zawadi ya mchezaji bora chipukizi (best rookie) ilichukuliwa na Pendo Laizer wa Orkeeswa. Zawadi ya kocha bora kwa timu za wanawake ilikwenda kwa Bariki Kilimba wa Fox Divas. 

Kwa upande wa wanaume, zawadi ya mfungaji bora ilibebwa na Cheikh Dialo wa Dar City ambapo zawadi ya beki Bora ilichukuliwa na Mathew Mmasi huku tuzo ya mchezaji chipukizi ilikwenda kwa Feisar Mlanzi wa timu ya Pamoja na kocha bora ni Mohamed Mbwana wa timu ya Dar City. Washindi wa tuzo zote kwa wanawake na wanaume  walizawadiwa kila mmoja sh300,000.

Mbali na zawadi hizo, wachezaji na makocha mbalimbali walikuwa wanazawadiwa fedha kupitia Locker Room Bonus (LRB) Sh140,000 kila mmoja kutoka chapa ya betPawa ambayo ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo, Waziri wa Madini Anthony Mavunde alipongeza washindi na timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyokuwa na hamasa kubwa.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawapongeza wadhamini wakuu  betPawa ambapo kwa kupitia mpango wa Locker Room Bonus (LRB) umeyafanya mashindano haya kuwa na ushindani mkubwa,” alisema Mavunde.

Vilevile aliishukuru Azam TV kwa kuhakikisha Watanzania wote nchini wana kufuatilia mashindano hayo kwa ubora wa kimataifa. 

Kwa upande wake, Mratibu wa Masoko wa chapa ya betPawa wa Afrika Mashariki Nassoro Mungaya naye alimpongeza Waziri Mavunde na serikali kwa ujumla kwa kuchangia maendeleo ya michezo nchini na kuwavutia wadhamini kama kampuni yao.

Mungaya alisema kuwa betPawa imeendelea kuwa mshirika wa karibu wa mpira wa kikapu nchini, na msimu huu wamewekeza Sh317 milioni kwa ajili ya ligi ya NBL.

“Kipengele kikubwa kinachotambulisha udhamini wetu ni Locker Room Bonus (LRB) – mfumo wa kipekee barani Afrika unaowalipa wachezaji Sh140,000 papo hapo baada ya kila ushindi.

Tumeona kwa macho yetu namna LRB ilivyobadilisha ari ya wachezaji, kuongeza ushindani, na kuleta hamasa toka hatua za makundi hadi playoffs. Tunajivunia kuona uwekezaji huu umetoa matunda kwa timu bora kwani  mchezo umeimarika, na wachezaji wamethaminiwa, kwa kupata LRB, ” alisema Mungaya.

Alisema kuwa  chapa yao pia imechangia Sh13 milioni kwa ajili ya zawadi za washindi na tuzo mbalimbali. 

“Unaweza kuona jinsi gani chapa ya betPawa ilivyo uthaminisha mpira wa kikapu. Uwekezaji wetu si kwenye ligi tu, pia ni uwekezaji kwa vijana, vipaji na mustakabali wa michezo nchini,” alisema.

Alisema kuwa  Tanzania ina historia kubwa ya vipaji katika mpira wa kikapu na betPawa imejipanga kuendelea kuwa sehemu ya safari ya kukuza mchezo huu kwa muda mrefu kwa kuleta ubunifu, motisha, na kwa kuzingatia ustawi wa mchezaji.

Waziri wa Madini Anthony Mavunde(wanne kutoka kushoto waliosimama)  na mratibu wa Masoko wa betPawa wa Afrika Mashiriki, Nassoro Mungaya (wa pili kushoto) wakimkabidhi kombe la ubingwa wa klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL”  nahodha wa timu ya Dar City Amini Mkosa (wa tano kushoto) mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Kisasa Heroes uliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. 

Mratibu wa Masoko wa Afrika Mashiriki wa chapa ya betPawa, Nassoro Mungaya (kushoto) wakimkabidhi kombe la ubingwa wa klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL”  nahodha wa timu ya Fox Divas mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Vijana Queens  uliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. 

Waziri wa Madini Anthony Mavunde akihutubia mara baada ya fainali ya mashindano ya klabu bingwa ya Tanzania “betPawa NBL”  yaliofanyika kwenye uwanja wa Chinangali, Dodoma. 

Wachezaji wa timu ya Fox Divas wakipozi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa la mashindano ya betPawa NBL yaliyomalizika mkoani Dodoma.

Wachezaji wakichuana katika mechi ya fainali ya mashindano ya betPawa NBL kati ya Fox Divas na Vijana Queens 

Wachezaji wakichuana katika mechi ya fainali ya mashindano ya betPawa NBL kati ya Dar City na Kisasa Heroes

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad