Na Khadija Kalili, Michuzi TV
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Alli Ussi amezindua Miradi saba sambamba na kuweka jiwe la msingi Klabu ya kupinga Rushwa Shule ya Sekondari Kisarawe Mkoani Pwani.
Ukaguzi wa miradi hiyo umefanyika leo Aprili 03, 2025 ikiwa ni muendelezo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Akikagua miradi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Alli Ussi amesema kuwa miundombinu ya mabomba ya maji yaboreshwe kwenye mbweni la wasichana Shule ya Kisarawe ili wanafunzi waweze kupata huduma hiyo.
Aidha Ussi baada ya kukagua mabweni hayo mawili ya wasichana ameridhika na kusema yamejengwa kwa kuzingatia viwango na manunuzi ya Nest .
Aidha katika ziara yake hiyo, Ussi pia amezindua miradi mingine muhimu ikiwa ni pamoja na Klabu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliyopo kwenye Shule ya Sekondari Kisarawe, Mradi wa Maji Kata ya Kibuta, pamoja na jengo la utawala na madarasa ya shule ya Madugike inayopatikana Manerumango.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu, Ussi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu ujao na kupiga kura kwa amani na kushiriki kwenye michakato ya kisiasa, ili kuchagua viongozi watakaowaongoza na kuwaletea maendeleo.
"Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anajihadhari na rushwa, iwe kwa kupokea au kutoa, ili tuweze kupigana nayo kwa pamoja," amesema Ussi.
Kwa upande wa Mradi wa Maji uliopo Kata ya Kibuta, Ussi amesisitiza kuwa wakandarasi wanatakiwa kumaliza mradi huo ndani ya wakati kama jinsi walivyosema kuwa wataukamilisha ifikapo Agosti mwaka huu ambapo tangi hilo la maji linauwezo wa kuhifadhi maji lita 90,000.
Akitolea mfano wa miradi mingine ya maendeleo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Seleman Jafo, amesema kuwa wananchi wa Kisarawe walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji, jambo lililosababisha serikali kuchimba kisima kirefu katika eneo hilo. Dkt. Jafo pia ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji unaoendelea.
"Serikali imejizatiti kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma ya maji kwa wakati, na leo tunashuhudia mafanikio makubwa katika mradi huu," amesema Dkt. Jafo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, amesema kuwa ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kisarawe umegharimu zaidi ya Mil. 137 fedha za ndani.
"Bweni hili litawapa fursa wanafunzi wa kike kusoma kwa amani na hatutakuwa na tena vikwazo vya muda mrefu wa kutembea kwa muda mrefu jambo ambalo pia litasaidia kupunguza mimba na ndoa za utotoni," amesema Magoti.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Wilayani Kisarawe umekagua miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1 . umekimbizwa umbali wa Kilometa 195 na kukagua jumla ya miradi saba ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti wakati akitoa taarifa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2025 katika Wilaya ya Kisarawe ukitokea Wilayani Kibaha katika viwanja vya Kiluvya madukani ambapo katika fedha hizo ni kutoka mapato ya ndani kutoka halmashauri ya Wilaya, kutoka Serikali Kuu, wahisani na nguvu za Wananchi.
Magoti amesema miradi itazinduliwa, mradi mmoja umewekwa jiwe la Msingi na miradi mitatu imekaguliwa
No comments:
Post a Comment