jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KUMBUKIZI YA MIAKA 53 YA KIFO CHA HAYATI KARUME

Share This

 

D8


D08

D008


D6

D5

D4

D3

D1

D01

6


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi katika Dua na Kumbukizi ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hayati Sheikh Abeid Amani Karume iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 Aprili 2025.

Kumbukizi hiyo imeongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Marais Wastaafu wa Zanzibar Mhe. Ali Mohamed Shein na Mhe. Amani Abeid Karume, Mjane wa Hayati Abeid Karume Mama Fatma Karume pamoja na familia ya hayati Karume.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara Mhe. Stephen Wasira, Viongozi, Wanachama na Wazee wa Chama cha Mapinduzi Viongozi wa Mahakama, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Dini mbalimbali
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad