Kampuni ya GF Trucks kupitia kampuni ya GF Automobile imeingia makubaliano na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini NaCoNGO ( The National Council of NGOs) akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo ,Mujtaba Karmali alisema katika makubaliano hayo yamelenga kunufaisha pande zote mbili
Wao kama wauzaji wa magari na mitambo waliona kuna haja ya kuingia makubaliano hayo ya kimkakati kupitia mkataba huo na kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kutoa Elimu,Kuwajengea uwezo na uelewa katika nyanja mbalimbali.
Pia Karmali amesema wao wameanza mpango wa kuwapatia mafunzo kazi kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali mfano , VETA na DIT ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi na kupata uzoefu kazini, Pia alisema Makubaliano hayo yatarahisisha kuwafikia Makundi ya vijana nchi nzima na kuungana na serikali katika mpango wa kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri kwa kupita katika vyuo mbali mbali.
Nae Mwenyekiti wa NaCoNGO , Jasper Makala ameishukuru Kampuni ya GF Trucks kwa kuonyesha njia kwa makampuni ya Kitanzania kuchangia maendeleo ya Jamii kupitia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali. Alisisitiza kuwa ushirikiano na makampuni binafsi ya ndani ya nchi ni mbinu mojawapo ya kupunguza utegemezi toka nje ya nchi kuelekea katika uendelevu wa Mashirika. @gftrucks
Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala wakionyesha nyaraka baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbali mabli ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini mkataba kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbali mabli ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.Wengine ni Katibu wa NaCoNGO ,Adamson Masimba (kushoto) na Kulia ni Afisa masoko wa GF Dianarose


Mkurugenzi wa Masoko wa GF Automobile ,Mujtaba Karmali akisaini makubaliano na Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala kwa ajili ya kushirikiana katika Nyanja mbalimbali ilikwamo utoaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa NaCoNGO nchini Tanzania , Jasper Makala akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika Nyanja mbalimabli na kampuni ya GF Automobile ilikwamo utaji wa Elimu na utaalamu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment