Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo, Steven Nyerere amesema kuwa Waziri Gwajima anatambua umuhimu wa Wanawake hasa kulinda utamaduni wetu na kukikumbusha kizazi hiki kulinda amani na kukemea vitu mbalimbali vinavyovunja utu.
Amesema kuwa "Dkt. Gwajima anatambua mchango wetu, kuanzia kampeni ya Samia nivushe kiatu, baiskeli ya mama na makundi ya walemavu".
Aidha amesema kuwa Kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani mwezi Machi taasisi ya mama ongea na mwanao itatoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha jambo la mama ni jambo letu.



No comments:
Post a Comment