jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

MMILIKI WA SALAAMAN HOSPITALI AHUKUMIWA

Share This

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani mmiliki wa Hospitali ya Salaaman Dkt. Abdi Warsame Hiris (60) Raia wa Canada mwenye asili ya Somalia na kuamuliwa kurudisha kiasi cha Sh. Milioni 24. 8 kama hasara aliyoisababishia Serikali wakati akiomba Uraia daraja C.


Pia Mahakama imemuhukumu kulipa faini ya Sh. 2,050,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu na miezi nane gerezani baada ya kupatikana na hatia katika makosa sita aliyokuwa akishtakiwa nayo. Yapo ya kutoa tamko la uongo.

Hukumu hiyo imesomwa leo Januari 30,2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Rahim Mushi.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mushi amesema upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo.

Akisoma adhabu Hakimu Mushi amesema mshtakiwa katika kosa la kwanza na la pili anatakiwa kulipa faini ya Sh. 25,000 kwenye kila kosa au kwenda jela mwezi mmoja wakati shtaka la tatu, shtaka la nne na shtaka la tano mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya sh. Laki tano kwenye kila kosa au kwenda jela miezi sita huku kwenue shtaka la sita mshtakiwa Warsame ametakiwa kulipa faini ya Sh. 500,000 au kwenda jela miezi sita.

Aidha mahakama imesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha hasara aliyoisababisha mshtakiwa kiasi cha Sh USD 10,000 na siyo USD 12,500 Kama ilivyo katika hati ya mashtaka na hivyo amemuamuru mshtakiwa kuilipa hasara hiyo kwa fedha za Tanzania ambazo ni sawa na Tsh. 24,865,000.

Pia ameamuru vibali vya mshtakiwa vya kufanya kazi visisitishwe kwani ni halali, mshtakiwa ni muwekeezaji na ameajiri watu wengi na pia inaonyesha mwaka 2023 alisajili vibali halali

Katika kesi hiyo inadaiwa mshtakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka matano ya kutoa matamko ya uongo wakati akiomba kibali cha ukaazi daraja C na shtaka moja la kuisababishia Idara ya Uhamiaji hasara ya zaidi ya USD 12,500

Katika shtaka la kwanza inadaiwa kati ya Julai 2014 na Oktoba 2014, huko katika ofisi za Uhamiaji, Kurasini mshtakiwa akiwa si raia na ni muwekwezaji, alitoa tamko la uongo kwa Kamisha Mkuu wa Uhamiaji wakati akiomba kibali cha makazi daraja C na kufanikiwa kupata kibali hicho kwa namba RPC1017007 huku akijua kwamba yeye ni muwekezji na mmiliki wa kampuni za Salaaman Health Service Limited na Salamaan Enterprises Ltd na hastahili kuwa na kibali cha makazi daraja C.

Pia mshtakiwa katika tarehe na miaka tofauti mwaka 2016, 2018, 2020 na 2021 alijipatia vibali kwa namba tofauti tofauti vya makazi wakati akijua yeye ni muwekezji na hastahili kupata vibali hivyo.

Katika shtaka la kuisababishia Serikali hasara, mshtakiwa anadaiwa kati ya Julai 2014 na Septemba 2021, Wilaya ya Temeke kwa makusudi alitoa tamko la uongo kwa Kamishna Mkuu wa uhamiaji wakati akiomba kibali cha makazi daraja c na kuisababishia uhamiaji hasara ya dola 12,500.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad