jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

GreenFaith imetoa wito kwa Viongozi wa Afrika, Yapongeza Juhudi ya Nishati safi

Share This

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Green Conservation inayojishughulisha na mabadiliko ya tabia ya nchi na Mazingira Ziada Kassimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2025.WhatsApp%20Image%202025-01-30%20at%203.16.14%20PM

 Afisa Mwandamizi wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi na nishati Jadidifu, Baraka Machumu katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2025. Kulia ni Mratibu wa taasisi ya Greenfaith Tanzania, Baraka Lenga na kushoto ni Mkulima wa Morogoro, Steven Selestin.
WhatsApp%20Image%202025-01-30%20at%203.16.11%20PM
Mratibu wa taasisi ya Greenfaith Tanzania, Baraka Lenga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2025.
WhatsApp%20Image%202025-01-30%20at%203.16.10%20PM
Kushoto ni Mkulima wa Morogoro, Steven Selestin akizungumza na waandishi wa habari juu ya Nishati Safi inavyotumika katika kilimo.
WhatsApp%20Image%202025-01-30%20at%203.16.06%20PM


JUMUIYA ya Asasi za Kiraia ya GreenFaith Tanzania imetoa wito kwa Viongozi wa Afrika na watunga sera kukataa ujumuishaji wa nishati ya nyuklia na gesi asilia katika ajenda ya nishati safi barani la Afrika.

"Badala yake, tunatoa wito wa kupewa kipaumbele kwa teknolojia jadidifu kama vile jua na upepo, ambazo siyo tu zinapunguza uzalishaji wa hewa chafuzi wa mazingira bali pia zinawawezesha wananchi kupitia uzalishaji wa nishati wa ndani, utengenezaji wa ajira pamoja na uimarishaji wa nishati stahimilivu."

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2025 na Mratibu wa taasisi ya Greenfaith Tanzania, Baraka Lenga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kufuati mkutano wa Nishati uliojumuisha viongozi wakuu wa nchi mbalimbali barani Afrika.

Amesema kuwa mpito wa nishati duniani unatoa fursa isiyo ya kawaida kwa Afrika kutatanua upya mustakabali wake wa nishati hata hivyo hili linapaswa kufanyika kwa njia inayotanguliza haki ya ushirikishwaji na uendelevu wake.

"Tunatoa wito kwa viongozi wa Afrika kuoanisha vipaumbele vyao ya nishati na misingi hii kwa kukataa suluhisho za uongo na kujitolea kwa mifumo ya nishati safi na endelevu." Amesema

Kwa Upande wa Afisa Mwandamizi wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi na nishati Jadidifu, Baraka Machumu amesema kuwa amesema kuwa mahitaji ni kuwekeza kwenye nishati mbadala kwasababu nishati kama ndio inayolinda na kutunza mazingira.

Amesema nishati ya Mafuta ni nishati inayosababisha watu wanyang'anywe ardhi kutokana na njia za upatikanaji wake na njia ya kuchimbwa ni inachochea mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kiasi kikubwa.

Machumu akitolea mfano Bomba la Mafuta linatotokea uganda hadi Tanga linaenda kuzalisha hewa ukaa kwa wingi kuliko kupunguza. Na ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira ni lazima kuwekeza kwenye nishati jadidifu ambayo haileti athari katika mazingira na kuleta haki sawa kwa wananchi.

Amesema juhudi za kuharakisha uzalishaji wa nishati safi zinastahili pongezi, ujumuishaji wa yanzo kamagesi na Nyuklia nishati ambazo zinaleta hatari kubwa zinazohatarisha uendelevu wake na uadilifu wa kijamii na kimazingira.

"Gesi Asilia si 'Nishati ya Mpito' bali ni Uongo Gesi asilia ambayo mara nyingi huuzwa kama mbadala safi, si endelevu wala safi. Uendeshaji wa gesi hutoa methane, gesi chafu yenye madhara mara 80 zaidi ya CO2 kwa muda mfupi, hivyo kuchangia kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya tabianchi. Zaidi ya hayo, uchimbaji wa gesi unaharibu mifumo ya ikolojja, unadhoofisha vyanzo vya maji, na kuathiri zaidi jamii za vijijini na watu waliotengwa." Amesema

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Green Conservation inayojishughulisha na mabadiliko ya tabia ya nchi na Mazingira Ziada Kassimu amesema kuwa Nishati ya gesi ni nishati inayowatenga watu kutokana na gharama zake wengine hawamudu kukunua nyingine mara inapoisha.

Pia amesema kuwa uwekezaji katika miundombinu ya gesi unazifungia nchi za Afrika katika utegemezi wa muda mrefu na na inachelewesha mpito kuelekea nishati jadidifu pia ni hatarisha kwa malengo ya tabianchi.

"Athari kwa Jamii na Haki za Mazingira uendelezaji wa nyuklia na gesi unashindwa kuzingatia hali halisi za maisha ya jamii za Kiafrika zinazobeba mzigo wa miradi hii, kuanzia watu kupoteza makazi yao kwa sababu ya bomba za gesi hadi

hatari za kiafya zinazosababishwa na taka za nyuklia, vyanzo hivi vya nishati vinachochea ukosefu wa haki za kimazingira na kuongeza ukosefu wa usawa." Amesema Ziada

Amesema jamii zilizo karibu na maeneo ya uchimbaji na hifadhi ya taka mara nyingi hutengwa kutoka katika mchakato wa kufanya maamuzi, hali inayokiuka misingi ya haki na usawa.

Kwa Upande wa Mkulima wa Morogoro, Steven Selestin, amesema kuwa Wakulima pia wanahitaji nishati safi kwaajili ya utunzaji wa mazao kwani nishati kama umeme unahitajika katika ulinzi pamoja na umwagiliaji.

"Kilimo cha sasa hakitegemei tuu maji ya mvua bali inategemea umwagiliaji pia ili kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Afrika kwa ujumla." Amesema
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad