JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WATENDAJI WA UBORESHAJI ZANZIBAR WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUFUATA SHERIA

Share This

 

Mjumbe wa Tuhe Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Uboreshaji ngazi ya majimbo katika mikoa yote ya Kisiwa cha Pemba, Zanzibar. Mafunzo hayo yamefungwa leo Oktoba o2, 2024 amewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Visiwani Zanzibar kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao.

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) akiwa meza kuu na viongozi wengine.


Mjumbe wa Tuhe Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magadalena Rwebangira akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Uboreshaji ngazi ya majimbo katika mikoa yote ya Kisiwa cha Unguja visiwani Zanzibar. Mafunzo hayo yamefungwa leo Oktoba o2, 2024 ambapo amewataka watendaji hao kutekeleza jukumu la kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kushiriki kwenye uboreshaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi.



Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima Ramadhani akizungumza jambo.

Mwenyekiti wa Mafunzo hayo akizungumza jambo kuhusiana na mafunzo hayo waliyopewa.



Sehemu ya washiriki kutoka mikoa yote ya Pemba wakimsikiliza mgeni rasimi wakati wa kufunga mafunzo hayo.



Sehemu ya washiriki kutoka mikoa ya Unguja wakimsikiliza mgeni rasimi wakati wa kufunga mafunzo hayo.


Sehemu ya washiriki kutoka mikoa ya Unguja wakimsikiliza mgeni rasimi wakati wa kufunga mafunzo hayo.



Sehemu ya washiriki kutoka mikoa ya Unguja wakimsikiliza mgeni rasimi wakati wa kufunga mafunzo hayo.



Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Visiwani Zanzibar kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omari Ramadhan Mapuri wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa TEHAMA kisiwani Pemba leo Oktoba 2, 2024.

Amewahimiza watendaji hao kuwahamasisha wananchi wenye sifa wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao.

“Ni matarajio ya Tume kuwa, mara baada ya zoezi hili kukamilika watu watakaokuwa wamepatiwa kadi watakuwa ni wapiga kura halali wa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Mhe. Balozi Mapuri.

Kwa upande wake Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Rwebangira amewataka watendaji hao kutekeleza jukumu la kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kushiriki kwenye uboreshaji kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi.

“Mabango na vipeperushi mtakavyopewa na Tume mvisambaze mapema katika shehia zote zilizopo katika mikoa yote mitatu ya Unguja. Kazi yenu kubwa ni kusimamia na kuendesha shughuli zote za uboreshaji katika shehia zote” amesema Mhe. Magdalena.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura visiwani Zanzibar umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 7 hadi 13 Oktoba, 2024 ambapo katika Ksiwa cha Pemba utafanyika katika mikoa miwili na Unguja katika mikoa mitatu.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mazoezi ya vitendo ya matumizi ya mashine za BVR ambazo zitatumika kusajili Wapiga Kura visiwani Zanzibar katika zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Oktoba 7 hadi 13 mwaka huu.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mazoezi ya vitendo ya matumizi ya mashine za BVR ambazo zitatumika kusajili Wapiga Kura visiwani Zanzibar katika zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Oktoba 7 hadi 13 mwaka huu.




Washiriki wakifanya mazoezi ya vitendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad