jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

TAWLA YAWAPIGA MSASA WANAHABARI

Share This

 CHAMA cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kinaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini ikiwa na lengo  la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/ utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii inayofanyika jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema waandishi wa habari wanabidi kuzingatia maadili na ubora katika kazi za uandishi ikiwemo na uzingatiaji wa sheria zilizowekwa.

"MCT itaendelea kushirikiana na wadau kama TAWLA ili kuhakikisha habari zinazohusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza zinafika kwa umma kwa lengo la kuhamasisha mapambano dhidi ya magonjwa hayo." alisema Sungura

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Wakili Tike Mwambipile amesema ukosefu wa mazoezi ni mojawapo ya sababu kubwa zinazochangia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile magonjwa ya moyo na kisukari. 

Pia ametoa wito kwa jamii kufanya mazoezi na kutumia vyakula bora kwa kuwa gharama kubwa zinatumika katika kutibu magonjwa yasiyoambukizwa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii
DSC_6178
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Wakili Tike Mwambipile akizungumza kuhusu historia ya kuanzishwa kwa chama hicho wakati wa mafunzo wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii.
DSC_6214
Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano, Afrika kutoka Global Health Advocacy Incubator (GHAI), Bobi Odiko akizungumza kuhusu lengo lao la kusaidia nchi na mashirika ya afya kuunda na kutekeleza sera zinazosaidia kuboresha afya ya umma kwa kutumia mbinu za kitaalamu na uhusiano mzuri na wadau muhimu ili kuhakikisha kwamba sera zinazotekelezwa zina athari chanya katika maisha ya watu.
DSC_6125
DSC_6126
DSC_6142
DSC_6195
DSC_6196
DSC_6200
DSC_6202
DSC_6221
Baadhi ya Wafanyakazi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) pamoja na waandishi wa habari wakifuatlia mada wakati wa mafunzo wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii.
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad