Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili, alieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu wa Septemba 2024. Lengo kuu ni kutatua tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwadui, sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita za kumtua mama ndoo kichwani.
Chanzo cha maji kwa mradi huo ni kisima kirefu kilichopo kijiji cha Nyankende, chenye uwezo wa kuzalisha lita 14,000 kwa saa. Mradi huu, ukiwa umekamilika kwa asilimia 85, utahudumia takriban wakazi 2,058 wa kijiji cha Mwadui na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 300.



No comments:
Post a Comment