Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KATIKA kipindi cha Julai hadi agost 2024 watuhumiwa saba katika mkoa wa Pwani, wamehukumiwa miaka 30 jela na wengine kufungwa maisha kwa makosa ya kulawiti, kubaka na kuzini .
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alieleza, wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Alitaja kati ya watuhumiwa hao ni pamoja na fundi magari na Mkazi wa Kiluvya, Kisarawe, Seleman Mirai Kibiki (49), ambae amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka saba huko Kiluvya kwa Komba, Kisarawe.
Alitaja wengine kuwa ni Yusuph Ngula Kitala (30), Mkazi wa Bagamoyo, miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka, Mtugani shaban Raim (45), Mkazi wa Bagamoyo, miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti”
“Hussein Abas Pontia (32), Mkazi wa Bagamoyo, miaka 30 jela kwa kosa la kuzini na maharimu, Gudulo Suma Manyawa (54), Mkazi wa Bagamoyo, miaka 30 jela kwa kosa la kubaka, Sijui Hashimu Kambunga (18), Mkazi wa Chalinze, jela maisha kwa kosa la kulawiti "
Lutumo alieleza, mtu mwingine ni Abdallah Diwani Dege (55), Mkazi wa Chalinze, miaka 30 jela kwa kosa la kujaribu kubaka, pamoja na Livinus Fortunas Kibate (34), Mkazi wa Chalinze, miaka 30 jela, kwa kosa la kubaka.
Kadhalika Lutumo alieleza, mtuhumiwa Selemani yeye baada ya kuhukumiwa alijinyonga akiwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe, wakati akisubiri kupelekwa gerezani mara baada ya kutiwa hatiani na Mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka na kulawiti Mtoto wake wa kufikia .
Amesema “Mara baada yakusomewa hukumu hiyo August 13,2024, Seleman aliingia chooni kisha kujinyonga kwa kutumia shati lake ambalo alilifunga kwenye nondo za dirisha la choo hicho, mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa uchunguzi wa Daktari na jana kukabidhiwa kwa Ndugu kwa ajili ya mazishi”
No comments:
Post a Comment