BALOZI wa Tanzania nchini Korea, Togolani Edriss Mavura ameambatana na wasanii aliowaalika kufanya ziara nchini Korea kusini na kukutana na msanii mkubwa nchini humo Ye-Jin kwa lengo kuimarisha mahusiano na kubadilishana ujuzi katika soko la filamu na kubadilishana mawazo ya namna ya kuendeleza sekta hiyo kimataifa.
Aidha wamekutana na na watengeneza filamu wakubwa Cheol-ha Lee na Yohwan KIM.
Director Cheol-ha Lee amesema yupo katika maandalizi ya filamu itakayohusisha waigizaji wa kimataifa’International’ na angependa kupata muigizaji kutoka Tanzania kwa Afrika.
Katika kikao hicho wasanii hao wametoa mawazo mbalimbali ikiwemo Serikali kuweka nguvu katika kuinua wasanii wadogo ili kukuza na kuendeleza vipaji.
Aidha wamepokea mwaliko kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuja Tanzania kuchagua maeneo mbalimbali ya kufanyia filamu zao na kisha kutembelea vivutio maridhawa vinavyopatikana Tanzania.
Wameshukuru kwa zawadi za shuka za kimasai walizovalishwa na kiongozi wa msafara Steve nyerere, msanii Irene Uwoya na Blandina Chagula (Johari).
Post Top Ad
WASANII WA TANZANIA WAKUTANA NA STAR WA KOREAN DRAMA ‘Son Ye-jin
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo-wajibu kwa Wananchi wa Zanzibar kuonyesha mshikamano katika kupigania haki zao za msingi
Othman MichuziDec 02, 2024WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA
Ahmad MichuziDec 02, 2024TPA YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA KWENYE SEKTA YA UMMA
Ahmad MichuziDec 02, 2024
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment