JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


CPA Kasore aweka mikakati ya VETA yakuwafikia wananchi kupata ujuzi

Share This

 

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akipata maelezo kuhusiana mafunzo ya urembo  yanayotolewa na Chuo cha VETA Shinyanga  wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya VETA katika kufikisha mafunzo ya ujuzi kwa watanzania wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akipata maelezo mafunzo ya Umahiri wa Wanafunzi katika uchoraji wa ramani za nyumba  wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akipata maelezo kuhusiana ubunifu wa mashine ya kumenya viazi vya Chipsi  wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

*Wastaafu nao waweza kupata mafunzo ya kuendesha maisha bila kutegemea mafao

 Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema kuwa Serikali ya Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imevutia wawekezaji wengi ambapo nguvu kazi hiyo Uwekezaji itatoka VETA.

CPA Kasore ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema kuwa katika maonesho hayo kuna Ubunifu wa Teknolojia mbalimbali ambazo zinakwenda kutatua changamoto katika sekta zote za kiuchumi.

Amesema kuwa baada ya kutambua kuwa kuna uwekezaji mkubwa wa viwanda wameanzisha fani ya Mechatronics ambapo wanaosomea kozi hiyo watakwenda huko kutokana na mitambo ya viwanda kuhitaji wataalam hao.

Amesema wanakwenda na Sera ya Serikali ya kuwa wanafunzi wote wanafika kidato cha nne ambapo watapata kusoma  mafunzo ya ujuzi hapo ndipo VETA kuwa na kutengeneza Walimu watakwenda kuwafundisha ujuzi.

CPA Kasore amesema kuwa vijana wa Tanzania katika maeneo yote vyuo vya VETA vimejengwa waende kupata mafunzo ya ujuzi ambapo watakuwa wameondokana na tatizo la ajira kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.

Amesema katika kuwa Kilimo ni Uti wa mgongo ambapo wanaotaka kufanya Kilimo watapata mafunzo na ujuzi na Kilimo cha uhakika na sio Kilimo cha kubahatishaa hali kadhalika kwa Sekta mifugo na Uvuvi wafanya hivyo hivyo.

Aidha amesema katika kuwa VETA katika kutambua changamoto ya makundi Maalum VETA inachukua na kupata mafunzo ambapo matokeo yake hadi sasa yamekuwa chanya na kutoa wito wa jamii kuacha kuwafungia ndani kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha fursa za msingi kwa kundi hilo.

" Sisi tunataka vijana wote nchini wapate ujuzi ambao unakwenda kuwa fursa yao katika kuendesha maisha yao kutokana kuwepo kwa mahitaji mengi ya ujuzi huo kutumika"amesema CPA Kasore.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imeendelea kuwekeza Ujenzi wa vyuo kuanzia Wilaya hadi Mikoa ikiwa na lengo ya kutoacha nyuma watu wote kwenye kupata mafunzo ya ujuzi.

CPA Kasore amesema kuwa Hadi wastaafu wanaweza kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kuendelea kuzalisha bila kutegemea mafao ya ustaafu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad