JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Wananchi wavutiwa na maroboti kwenye viwanja vya sabasaba

Share This

 


*Wataka Maonesho yaongezwe Siku

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
BAADHI ya wananchi waliofika katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wamesema Maonesho ya mwaka huu ni tofauti ikiwemo maboroboti ambapo hawajawahi kufikiria kuona ubunifu wa maboroboti hayo.

Maonesho yakiwa yamebakiza Siku mbili kufungwa maroboti hayo miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa kivutio kwa wananchi wanaotembelea Viwanja wa Sabasaba.

Katika moja ya eneo ndani ya Maonesho lenye maroboti limesababisha kujaza watu wengi.

Mmoja wa Mwananchi Joseph Shija amesema kuwa Sabasaba inautofauti wa aina yake na kutaka wananchi wengine watembelee.

Amesema ambapo maonesho yaongezwe siku huku wakiwataka watu yana raha na huduma mbalimbali zinapatikana.

Kwa upande wa Valentino Kivike Mkazi wa Kigamboni amesema maonesho ni mazuri maroboti yamekuwa kivutio sana na kudai kuwa vitu hivyo vitafanyika nchini na sio kuangalia katika maonesho

“Kwa mara ya kwanza ndio naona teknolojia mpya,naona yanaweza haya maroboti yanaweza kufaa hata kwenye kazi na mambo mengine.

“Hii inaonyesha inaweza kufanya kazi yoyote kwa sababu nimeona anaweza kucheza hivyo anaweza kufanya na kazi nyingine lakini licha maroboti nimeona vitu mbalimbali vilivyomo ndani Sabasaba.”anasema Kivike.

Janeth Joseph Mkazi wa Kigamboni amesema roboti ni kitu kipya anaona ni kama sehemu ya mabadiliko katika maonesho hayo na kuongeza kuwa ametembelea mara ya tatu kutokana na kuwepo utofauti na Maonesho yaliyopita .

“Kuna watu hawajui Sabasaba kwa sababu wanahisi hakuna kitu kipya cha kujifunza lakini wanapaswa kujua kuwa ukija huku utapata burudani ,unatengenwz afya ya akili,”amesema.

Amesema ni wakati serikali kutoa nafasi zaidi kwa wabunifu wa stadi za mikono na bunifu nyingine ili kuweka mazingira tofauti.

Ameiomba serikali kuongeza siku za maonesho kutoka Julai 13 yaishie Julai 20.

Maonesho hayo Sabasaba yalianza rasmi Juni 28 na yatarajiwa kumalizika Julai 13 ambapo kwa mwaka huu yalizinduliwa na Rais wa Msumbiji Jancito Nyusi akiongozwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad