JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MTAFITI WA SOKWE AISHUKURU COSTECH, 'IDADI YA SOKWE INAPUNGUA'

Share This

 


KATIKA kuelekea siku ya Sokwe duniani inayoadhimishwa kila mwaka Julai 14, 
Mtafiti kutoka Taasisi ya Dk Jane Goodall (JDI) amesema kuwaidadi ya sokwe katika Hifadhi ya Taifa Gombe,inapungua kutoka 150 hadi 85 kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo  Julai 11, 2024, mtafiti wa Sokwe, Dkt. Jane Goodwall alipotembelea Ofisi za Tume ya Sayansi Tanzania (COSTECH) kushukuru kwa Ushirikiano waliompa wakati akifanyatafiti amesema Sokwe hao wanapungua kutokana na milipuko ya magonjwa na shughuli za kibinadamu zinazofanyika kwenye hifadhi hiyo pamoja na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.

Dkt. Jane pia ameshauri kulindwa kwa mnyama huyo adimu duniani.

Amesema kuwa amefanya utafiti kuhusu tabia na maisha ya sokwe waliopo hifadhi ya Gombe kwa miaka 65 na kwamba eneo hilo ni miongoni mwa makazi machache yaliyosalia ya sokwe mtu duniani.

"Wakati naanza kufanya utafiti katika hifadhi ya Gombe ilikuwa na sokwe kati ya 120 hadi 150 na mpaka sasa idadi yao imepungua kwa sababu ya magonjwa ya njia ya hewa wanayoyapata kutokana na muingiliano wao na binadamu." Amesema

Ameeleza kuwa kuna magonjwa mengine ya mlipuko na ya asili ambayo hutokana na muingiliano kati yao na binadamu na husambaa kwa njia ya hewa kama Mafua.

" Wakati huo Msitu ulikuwa na uwezo wa kuwapatia sokwe chakula cha kutosha hivyo hawakuwa wanaenda nje ya hifadhi lakini kutokana na shughuli mbalimbali za binadamu, huwafanya sokwe kwenda nje ya hifadhi hiyo kutafuta chakula."

Amesema kuwa katika kufanya Utafiti huo wanashirikiana na serikali za vijiji kwa ajili ya kuongeza uhamasishaji wa kutunza hifadhi hii lakini pia kuwepo kwa ushoroba wa msitu kutoka Kaskakazini hadi Kusini mwa hifadhi hii ambayo ni karibu na Burundi kutasaidia sokwe kuwa na uwezo wa kubadilishana vinasaba na sokwe wengine waliokaribu na hifadhi.

Dkt. Jane ameeleza namna ya kufadhi mazingira na kupunguza shughuli za kibinadamu ili ktaleta faida kwa wanyama wengine lakini pia itawezesha kizazi kijacho kushuhudia sokwe watu.

Mtafiti huyo amesema kadri idadi ya binadamu inavyoongezeka na misitu inapungua hivyo idadi kubwa ya sokwe hugawanyika na kupunguza utofauti wa kijeni na uwezekano wa kuishi kwa muda mrefu kwa kila jamii.

‘’Taasisi ya Jane Goodall inaamini kwamba njia bora ya kulinda makazi yenye afya ni kuzingatia vitendo ambavyo sio tu vinalinda wanyama walio hatarini na makazi yao, lakini pia kunufaisha watu wa eneo hilo ambao maisha yao yanategemea mazingira bora,’’ alisema.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt Amos Nungu amesema "Leo nimetembelewa na watafiti kutoka hifadhi ya Gombe wanaofanya utafiti wa Sokwe utafiti huu ni mkubwa na wa muda mrefu ambao umetoa matokeo ambayo yamebadiri taswira ya mahusiano ya binadamu na wanyama kwa dunia nzima"

Amesema kuwa utafiti huo wa Sokwe ni wa muda mrefu toka ulipoanzishwa na Mtafiti mwandamizi na muanzilishi wake Dkt. Goodall ambaye amefikisha miaka 90 sasa.

Utafiti wa sokwe ni miongoni mwa tafiti mbalimbali ambazo wanazitolea vibali na hata kuzifadhili moja kwa moja.
mtafiti wa Sokwe, Dkt. Jane Goodwall  akizungumza alipotembelea Ofisi za COSTECH leo Julai 11, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2024 walipotembelewa na Mtafiti wa Sokwe, Dkt. Jane Goodwall.




Baadhi ya washiriki walifika wakati Mtafiti Dkt. Jane Goodwall alipofika COSTECH leo Julai 11, 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad