JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Kipenga cha kumsaka gwiji wa Fasihi Afrika chapulizwa

Share This

 

PAZIA  la shindano la kumtafuta gwiji wa fasihi katika ukanda wa Afrika linalodhaminiwa na SAFAL Group kupitia kampuni zake tanzu za ALAF Limited (Tanzania) na Mabati Rolling Mills (Kenya) limefunguliwa .

Akizungumza na waandishi wa Habari, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa ALAF Tanzania, Hawa Bayumi alisema “ni fahari kubwa kwetu kuendeleza udhamini wa tuzo hizi zinazolenga kukuza fasihi na lugha ya kiswahili kwa ujumla. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazokuwa kwa kasi kubwa duniani na kutumika nchi kadhaa Afrika na duniani hivyo SAFAL Group ikiwa mzalishaji wa suluhishi bora za ujenzi barani Afrika hii imekuwa moja ya njia zetu muhimu za kuwajibika kwa jamii. Tunatambua lugha kuwa nyenzo muhimu ya ustawi wa uchumi na jamii hivyo tutaendelea kuwa wadau muhimu katika kukuza kiswahili.“

Tuna fahari kubwa kuendelea kufadhili Tuzo za Fasihi ya Kiswahili kwa Afrika ambazo zinalenga kukuza fasihi ya Kiswahili na lugha kwa ujumla. Kiswahili ni moja ya lugha zinazokua kwa kasi duniani na inatumika katika nchi kadhaa za Afrika. Safal Group inatambua umuhimu wa lugha kama chombo muhimu kwa maendeleo ya kitamaduni,kijamii na kiuchumi. Tutaendelea kukuza ukuaji wa fasihi ya Kiswahili kupitia mashindano haya.‘‘

Aidha aliongeza kwa kusema shindano hili litahusisha miswada ambayo haijachapishwa, katika tanzu za riwaya na ushairi ambapo zawadi za jumla ya Dola 15,000 za Marekani zitatolewa kwa washindi mbalimbali. Vitabu vilivyokwisha chapishwa havitazingatiwa.

Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 2014 na Dkt. Lizzy Attree na Dkt. Mukoma wa Ngugi ili kutambua uandishi kwa lugha za Kiafrika na pia kuhimiza tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe. Tuzo hii imewezesha miswada ya washindi 24 kuchapisha kazi zao kuwa vitabu kupitia mchapishaji Mkuki na Nyota. Nakala zapatikana kupitia https://mkukinanyota.com/shop/. Kupitia ufadhili wa Safal Group, zaidi ya vitabu 4,000 kutoka kwa waandishi walioshinda vimechapishwa na kusambazwa katika taasisi za kujifunza na maktaba nchini Tanzania na Kenya.

“Wakati juhudi za kuhimiza kusoma na kuandika kwa Kiswahili zinaendelea, tunawahimiza waandishi kutoka Afrika Mashariki na nchi nyengine za Afrika kuwasilisha miswada yao na kushiriki katika shindano la mwaka huu," aliongeza Hawa.

Tofauti na fedha taslimu, miswada itakayoshinda itachapishwa kuwa vitabu na shirika la uchapishaji la Mkuki na Nyota (Tanzania), ambalo linaweza kushirikiana na wachapishaji wengine ili kurahisisha upatikanaji wa vitabu vilivyoshinda. Vitabu vya ushairi vitakayoshinda vitafasiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa na Africa Poetry Book Fund.

Tuzo za mwaka 2024 zitatolewa Julai 2025, na waandishi wote walioorodheshwa watahudhuria.

Shindano hilo linatarajia kufanyika kwa msimu wa tisa sasa.

Miswada inaanza kupokelewa leo na zoezi hili litandelea mpaka tarehe 30 Novemba 2024 litakapofungwa kupisha mchakato utakaowezesha kupatikana washindi.

Safal Group ni mzalishaji na msambazaji mkubwa zaidi wa suluhisho za bidhaa ujenzi zenye ubora wa hali ya juu barani Afrika. Safal Group inauzalishaji katika nchi tisa za Afrika mashariki na kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad