JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KETI JIFUNZE YA BENKI YA CRDB YAZIFIKIA SHULE TATU MKOANI PWANI

Share This

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera (watatu kulia), amemkabidhi Mariam Kihiyo, Afisa Elimu wa Wilaya ya Chalinze (watatu kushoto), viti na meza ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Keti Jifunze ya Benki ya CRDB, ambayo lengo lake ni kutoa madawati kwa shule za Msingi na Sekondari nchini kote, katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Shule ya Msingi Ridhiwani Jakaya Kikwete, Chalinze, iliyopo Chalinze mkoani Pwani.
 
Vifaa hivi vimetolewa kwa shule tatu katika Mkoa wa Pwani ambapo kila shule ilipata seti ya viti na meza 50 kila moja. Benki ya CRDB imetoa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya sera yake ya kurudisha kwa jamii asilimia moja ya faida yake kila mwaka. 
 
Shule zilizofaidika na viti na meza hizi ni Shule ya Msingi Ridhiwani Jakaya Kikwete, Chalinze, Shule ya Sekondari Samia Mtongani, Mlandizi, na Shule ya Sekondari Shushila Ladwa, Bagamoyo. 
 
Mchango huu unalenga kusaidia serikali katika kutatua sehemu ya changamoto za elimu nchini.
Afisa Elimu wa Wilaya ya Chalinze, Mariam Kihiyo (katikati) akiwa pamoja na Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, George Yatera (kulia), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Chalinze, Exaud Mtui sambamba na sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ridhiwani Jakaya Kikwete, Chalinze mkoani Pwani, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera (kulia), akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi viti na meza katika Shule ya Msingi Ridhiwani Jakaya Kikwete, Chalinze, Pwani hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Faraja Kaziulaya.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad