JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KAMBI MAALUMU YA UDAHILI WA PAPO KWA PAPO YAANZA MZUMBE, UPANGA

Share This

 





Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakidahili wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa ngazi zote za elimu.

CHUO  Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam kuanzia Julai 15-21,2024 kimeweka kambi maalumu ya udahili wa papo kwa papo kwa wahitimu wote wanaotarajia kujiunga na Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kwa ngazi zote za elimu.

Akizungumza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Lulu Mussa amesema maafisa udahili wa Chuo Kikuu Mzumbe wameweka kambi maalumu katika ndaki ya Dar es Salaam ili kuwarahisishia wahitimu katika zoezi la udahili wa papo kwa papo.

Amesema mhitimu atapata nafasi ya kufanyiwa udahili wa papo kwa papo katika ngazi zote za elimu kuanzia astashahada, stashahada, shahada za awali, shahada ya umahiri na shahada ya uzamivu (Phd).

Mbali na udahili wa papo kwa papo, amesema mhitimu aliyepo mbali anaweza kuingia na kutuma maombi yake moja kwa moja kupitia admission.mzumbe.ac.tz au kupiga Namba 0752484810, 0756730733, au 0754532247 kwa msaada wa haraka wa namna ya kutuma maombi.

Ameongeza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimebobea katika kutoa mafunzo yake kwa vitendo zaidi ili kuandaa wataalamu mahiri katika kada mbalimbali ikiwemo TEHAMA, Biashara, Uhasibu na Fedha, Takwimu Tumizi, Utawala, Uchumi na Sheria.

Mmoja ya waliojitokeza kufanya udahili kwa ngazi ya Shahada ya Umahiri Bi Diana Luteganya amepongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuweka kambi ya udahili kwani imemsaidia kufanya maombi hapo kwa hapo bila kupotenza muda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad