JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


CHALINZE MODERN ISLAMIC WAFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO HOSPITALI YA RUFAA TUMBI

Share This

  







Na Khadija Kalili Michuzi Tv
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Mchepuo wa Kiingereza ya Chalinze Modern Islamic wamefanya ziara ya masomo kwa siku moja na kujifunza mambo mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Mwalimu wa Somo la Sayansi Rashid Hamisi Stambuli amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa Hospitali ya rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani kwa kuwapa fursa wanafunzi hao ambao ni Madaktari Tarajai kwani wameweza kutimiza lengo letu kwa asilimia 99% katika masomo ya Sayansi wanayosoma shuleni hapo.

"Hii ni mara ya ya kwanza Shule yetu kupata nafasi ya kupata ziara ya kimafunzo kwa vitendo wanafunzi wetu wenye ari ya kuja kuwa madaktari wetu wa baadaye wametembelea idara tatu ambazo ni Dharura, Idara ya kuchuja Figo na Wodi ya Watoto kuanzia umri wa siku sifuri hadi siku 28.

Akizungumza na wanafunzi hao Daktari Bingwa wa Watoto wadogo Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Dkt. Pius Muzzazi amebainisha kuwa miongoni mwa magonjwa yanayowaathiri watoto wadogo ni kuwa ni pamoja na kuwa na ukosefu wa afya ya akili unaosababishwa na malezi mabovu kutoka kwa baadhi ya wazazi ikiwa ni pamoja na kuwafokea na kuwatolea kauli zisizofaa.

"Watoto wengi wamekua wakipata msongo wa mawazo kutokana kupata maneno yasiyostahili kutoka kwa watu wao wa karibu na wanao wazunguka" amesema Dkt.Muzazzi.

Wakiwa katika ziara hiyo Muuguzi wa zamu kitengo cha kusafisha Figo Joyce Mfyuji amesema kuwa jamii nzima inapaswa kubadili mtindo wa ulaji kwa sababu ndiyo chanzo kikubwa cha kuharibu figo na kusisitiza kwamba endapo mtu ataupata ugonjwa huo itamlazimu kuchuja figo kwa kusafisha damu mara tatu kila wiki katika muda wote wa maisha yake.

Mwanafunzi Mussa Swedi amezungumza kwa niaba ya wenzake waliopata fursa katika ziara hiyo ya kimafunzo amesema kuwa amejifunza kuwa siyo kila mgonjwa huwa anapelekwa moja kwa moja kwenye wodi za watu maalumu (ICU),"nimejifunza kwamba mgonjwa wa dharura anapofika hupokelewa na kupewa huduma pia nimejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamojana kutambua kuwa kiungo kinachoitwa figo ni muhimu sanakatika maisha ya binadamu hivyo watu wote tunapaswa kukilinda kwa kuzingatia kula mko kamili, kufanya mazoezi.

"Pia nimefurahi kuonanamnamgonjwa akipatiwa huduma ya kusafisha damu hili limetujenga zaidi na kuona kaI ya Utabibu inahitaji uwe na moyo wa kujito zaidi"amesema Mussa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad