JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Afya ya Akili Inavyowatesa waathirika wa VVU

Share This

Mshauri wa masuala ya ya uzazi wa mpango (wa kwanza kulia)  Dkt. Emiliana Mswa, Mshauri Mwandamizi wa Maendeleo ya vijana, Angasyege Kibona wa katikati na Mshauri Mwandamizi wa EGPAF, Dkt. Juma Songoro wakiwa katika mkitano huo. 

Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la EGPAF nchini, Dkt. Sajida Kimambo (wa Pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mshauri Mwandamizi wa Maendeleo ya vijana, Angasyege Kibona (wa kwanza kushoto),  Akivila Temu, Mshauri wa masuala ya watoto (wa kwanza kulia) na Mshauri Mwandamizi wa EGPAF, Dkt. Juma Songoro wakati wa mkutano wa 25 wa kimtaifa wa wadau wote duniani wanaoshughulika na masuala ya Ugonjwa wa ukimwi.  Mkutano huo wa wiki moja unafanyika nchini Ujerumani katika jiji la Monic
Mshauri Mwandamizi wa EGPAF, Dkt. Juma Songoro akiwaelezea wadau wanaoshiriki mkutano wa 25 wa kimataifa wa masuala ya VVU na UKIMWI duniani namna ya kuawafanyia WAVIU uchunguzi wa afya ya akili ambayo ni afua muhimu jumuishi kwenye huduma tiba na matunzo kwa WAVIU.

Changamoto ya Afya ya Akili kwa Waathirika wa VVU*

IMEELEZWA kuwa Changamoto ya afya ya akili ni moja ya kikwazo kinachokwamisha maendeleo ya afya kwa baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (VVU) .

Hayo yamesemwa na Mshauri Mwandamizi wa EGPAF, Dkt. Juma Songoro, ambaye amehudhuria mkutano wa 25 wa International Aids Society (IAS) unaofanyika jijini Munich, Ujerumani. 

"Nimepata fursa ya kushiriki mkutano huu mkubwa na kuwasilisha mada kuhusu utoaji wa huduma ya uchunguzi wa afya ya akili kwa waathirika wa VVU. Tumefungua vituo 11 vya mfano na kuanza kutoa huduma hii ya uchunguzi katika huduma zetu za tiba na matunzo kwa WAVIU," amesema Dkt. Songoro.

Amesema kuwa wasilisho hilo limeangazia njia bora za kuwasaidia watu wenye changamoto za afya ya akili, hasa wale wanaokumbwa na msongo wa mawazo (depression) na wasiwasi uliopitiliza (anxiety). Hii inawawezesha kuwa wafuasi wazuri wa huduma za tiba na matibabu zinazotolewa bure na serikali. 

"Tumeonyesha uwezekano wa kuwasaidia kupitia uchunguzi wa afya ya akili kwa kutumia dodoso maalum, hasa kwa wale wanaoanzishiwa matibabu (ART) lakini wanashindwa kupunguza virusi, walioacha huduma za tiba na matunzo bila sababu maalum, na WAVIU wenye ujauzito au wanaonyonyesha ambao mara nyingi matatizo yao ya afya ya akili huwafanya kutokuwa wafuasi wazuri wa matumizi ya ARV. Wahudumu wa afya wanaweza kutoa dawa vizuri lakini virusi havipungui kwa sababu ya matatizo ya afya ya akili. Ukibaini na kutibu matatizo haya utaona maboresho,” amesema.

Dkt. Songoro amesema kuwa taasisi yao ilibaini changamoto hii na kuanzisha huduma ya uchunguzi kwa kuwajengea uwezo wahudumu katika vituo 11 vya afya vya mfano katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, na Singida. Walifanikiwa kuwafikia zaidi ya WAVIU 1,800 ambao walipatiwa uchunguzi wa afya ya akili na kubaini takriban 760 walikuwa na dalili za matatizo ya afya ya akili, wengi wao wakisumbuliwa na msongo wa mawazo na wasiwasi uliopitiliza ambao walipatiwa matibabu kutoka kwa wataalam wa afya ya akili katika vituo hivyo.

"Tulichobaini ni kuwa vijana wa kiume wenye umri wa miaka 10 hadi 19 wanakumbwa sana na msongo wa mawazo, wakati wasichana wenye umri huo wanakumbwa zaidi na wasiwasi uliopitiliza," amesema Dkt. Songoro.

Amesema takwimu hizi zinatokana na vituo 11 pekee kati ya zaidi ya vituo 500 wanavyosimamia huduma za tiba na matunzo katika mikoa hiyo mitano. 

Ni muhimu kutibu matatizo ya afya ya akili kwa sababu watu wengi wanapojigundua kwa mara ya kwanza kuwa wameathirika, wanakumbwa na msongo wa mawazo unaosababisha kushindwa kutumia dawa kupunguza makali ya VVU, kuambukiza wengine, na kuleta matatizo kwao na jamii inayowazunguka.

Dkt. Songoro ameongeza kuwa ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kumesababisha changamoto mpya katika kupambana na VVU. "Mbali na kutoa dawa, tunahitaji kutoa elimu kuhusu uzazi kwa waathirika na jinsi ya kuishi na VVU huku wakipatiwa tiba stahiki kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari, kansa, na matatizo ya afya ya akili," amesema.

Mkutano huu mkubwa umewakutanisha wataalam wa tafiti, waathirika wa VVU, watoa huduma, na wanaharakati mbalimbali. Dhamira kuu ya mkutano huu ni kuwaleta pamoja wadau wanaojihusisha na masuala ya VVU. Tafiti mbalimbali zinawasilishwa, ikiwa ni pamoja na kutafuta tiba, kinga, dawa mpya za kufubaza makali ya VVU, na utafiti wa chanjo unaoendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad