JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WIZARA YAITAKA NIRC KUSIMAMIA MAONO YA RAIS DK.SAMIA

Share This

 Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omar, amesema matarajio ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona sekta ya kilimo inaleta mageuzi ya kiuchumi nchini.

Amesema kutokana na hatua hiyo ni lazima kufanyia kazi changamoto zilizopo katika sekta ya umwagiliaji ili kuwa na matokeo hayo.

Dkt. Hussein ameyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Kamati zinazohusika na mradi wa Uhimilivu wa Mifumo ya Chakula unaodhaminiwa na Benki ya Dunia (WB).

Akieleza zaidi amesisitiza iwapo serikali haitafanyia kazi mahitaji yaliyopo katika sekta hiyo ya Umwagiliaji hakutakuwa na matokeo katika mageuzi ya kiuchumi yanayotokana na sekta ya kilimo nchini na wizara inaamini utendaji na ufanisi wa Tume unaweza kusimamia na kufikia azma ya Rais ya sekta ya kilimo kuleta mageuzi ya kiuchumi.

"Mradi huu ni muhimu katika mabadiliko ya tabianchi ili kuwa na usalama wa chakula, hivyo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inalo jukumu mahususi katika kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika mradi huu na kufikia maono ya Rais Dk. Samia sekta ya kilimo kuleta mageuzi ya kiuchumi,”amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhakiki Ubora, Naomi Mcharo, akitoa ufafanuzi katika mkutano huo amesema mradi huo ni wa dola za Marekani milioni 300 na unahusisha Awamu mbili moja wapo ikiwa ni Matokeo Kwanza (P4R) ukiwa ni utekelezaji wa miaka mitano.

Aidha Tume imetengewa Dola milioni 70 kufanikisha mradi huo kipindi hicho na kufafanua katika usimamizi na maamuzi ya mradi kunahitaji kuwa na kikao cha wataalamu, Kamati ya watendaji wakuu wa Wizara ambao ni Makatibu Wakuu wa Wizara katika sekta ya kilimo na kikao cha pande mbili za Muungano.

Amesema lengo ni kuangalia, kushauri na kuelekeza utekelezaji wa mradi ili kuleta ufanisi."NIRC imejipanga kukarabati miundombinu ya umwagiliaji kupitia mradi huo, kuwawezesha na kuwaelimisha wakulima juu ya uendeshaji, matunzo na usimamizi wa skimu za umwagiliaji."




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad