JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KANISA LA ANGLIKANA LA MT. ALBANO KUANDAA MBIO ZA WALKAMALA ZITAKAZOFANYIKA JUNI 22, 2024, KUSAIDIA JAMII YA WALEMAVU

Share This

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya WALKAMALA 2024, Nkela Makoko Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024 kuhusuana na mbio za WALKAMALA pamoja na Uchangishaji fedha kwajili ya kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu.
Kasisi Kiongozi wa Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano, Canon Jacob Kahemele katikati Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024 kuhusuana na mbio za WALKAMALA pamoja na Uchangishaji fedha kwajili ya kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu.
Mtu asiyeona, Noel Gumbo ambaye pia ataongoza matembezi ya WALAMALA katikati Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024 kuhusuana na mbio za WALKAMALA pamoja na Uchangishaji fedha kwajili ya kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu. kushoto ni Kasisi Kiongozi wa Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano, Canon Jacob Kahemele na Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya WALKAMALA 2024, Nkela Makoko.



Mratibu wa Kamati ya Ufundi wa Mbio za WALKAMALA, Joseph Katembo wa Pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na njia watakazopita watembeaji pamoja na wakimbiaji katika mbio za WALKAMALA zitakazofanyika Juni 22, 2024 jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na Ulaji mbovu Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano la jijini Dar es Salaam linatarajia kuandaa mbio za WALKAMALA 2024 zitakazofanyika Juni 22, 2024 jijini Dar Es Salaam.

Mbio hizo ni kwaajili ya kukusanya shilingi bilioni mbili kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Jamii na kusaidia watu wenye ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 25, 2024 Kasisi Kiongozi wa Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano, Canon Jacob Kahemele amesema kuwa wameona kuandaa WALKAMALA marathon ili kuungana na Serikali kuhamasisha jamii kwamba mbio hizo zitasaidia afya watu.

"Tunajamii ya watu wenye ulemavu tofauti tofauti inayotuzunguka ambao wanapitia magumu wakati mwingine inauhitaji wa kipekee sana sio baraka hizi wazipate wachache tukio kama hili la WALKAMALA linatusaidia sisi kupata baraka kutoka kwa Mungu."

Licha ya hayo pia Juni 22, 2024 itakuwa ni maadhimisho ya miaka 90 ya Kanisa la Mtakatifu Albano lililopo Posta jijini Dar es Salaam na kutakuwa na harambee ya ukusanyaji fedha.

Pia amewaomba watanzania kushiriki katika matembezi ya WALKAMALA ambayo yamepewa jina la Ochien and Gumbo WALKAMALA 2024 kwa sababu yanaongozwa na watu wenye ulemavu.

Pia amewakaribisha wananchi kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 90 ya kanisa hilo pia katika matembezi yatakayofanyika Juni 22 na kwenye uimbaji utakaofanyika kanisani hapo na katika ibada ya Juni 22 mwaka huu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya WALKAMALA 2024, Nkela Makoko amesema kuwa katika Matembezi hayo na WALKAMALA kutakuwa na 'KIT', nyenye gharama za shilingi elfu 35 ambayo itapatika Mlimani City na katika Kanisa la Anglikana la Mt. Albano Posta.

Pia kutakuwa na 'tracksuits' zitakazouzwa kwa shilingi 120,000/# ... "Tunawakaribisha watu wote kushiriki na kununua Vifaa visaidizi katika matembezi ambazo itakuwa ni sehemu ya kuchangia matembezi hayo."

Akizungumzia njia zitakazotumika katika Matembezi hayo pamoja na WALKAMALA, Mratibu wa Kamati ya Ufundi wa Mbio za WALKAMALA, Joseph Katembo amessema kuwa kutakuwa na mbio za Kilomita 5,10 na 21.

Mbio zote hizo zitaanzia katika Viwanja vya Farasi Maarufu The Gree Msasani na kumalizikia hapo hapo.

Pia amewaalika watanzania wote kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa yanayosababishwa na ulaji mbovu ili tuwaunge mkono watu wenye ulemavu walioonesha nia katika hali zao.

"Sisi tuliowazima tumshukuru Mungu kwa kuwaungamkono hawa wenzetu wenye ulemavu tuweze kutoa kwa moyo hata kama mtu hatashiriki mbio hizo ila kama mtu anawiwa kutoa atoe ili kutimiza malengo ambayo kanisa kwa ujumla imeyaweka lakini pia kuwagusa wahitaji." Amesema Katembo

Pia ameeleza jinsi ya kujisajili kunalipa namba ya tigo ambayo itatumika kwa mitandao yote kufanya malipo njia nyingine ni njia ya Benki ya CRDB.

"Pia kuna mfumo wa namna ya kujisajili pamoja na namba ya kutuma maelezo ya jina na umbali unaotaka kukimbia, Size ya Tisheti."

Kwa Upande wa Mtu asiyeona, Noel Gumbo ambaye pia ataongoza matembezi hayo amesema kuwa ameamua kufanya Matembezi hayo kwasababu Mungu yupo ndani yake katika Matendo ya jamii na kurudisha shukrani kwa Mungu.

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wanaweza wakiwezeshwa na kusikia wakisikilizwa pamoja na kutenda.

Pia amewakaribisha watanzania wote wa ndani na nje ya nchi, mashirika na makampuni... "Karibuni sana Kuniunga mkono kupitia mimi na kupitia Mwenyezi Mungu ili kuweza kuadhimisha miaka 90 ya kanisa la Mt. Albano."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad