JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Furahika yaweka mikakati ya kutoa Bima ya Afya bure kwa wanafunzi

Share This

 


Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Furahika Dkt.David Msuya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ,jijini Dar es Salaam.

*Yatoa kongole kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufingua milango katika ufadhili wa elimi nchini

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

CHUO cha Ufundi  Stadi cha Furahika kimejipanga kuwakatia Bima ya Afya wanafunzi wake wanaochukua kozi za mwaka mmoja ili kuwapa utulivu wa kutafuta matibabu wanapopata changamoto ya maradhi pindi wawapo chuoni hata wanapomaliza na kuanza kutafuta kazi au kujiajili.

Hayo ameyasema Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. David Msuya wakati akizungumza na waandishi habari kuhusu mikakati waliojiwekea kwenye Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Dkt.Msuya amesema kuwa kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wafadhili wamepanga kuanza na bima kwa wanafunzi 30 na siku zijazo idadi hiyo itaongezeka kulingana  na mahitaji na hao wanaoanza ni majaribio.

 “Haya kwetu ni mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa chuo hiki mwaka 2021, hata hivyo wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan (SSH) kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa kufungua milango kwa wawekezaji kuja nchini kuunga mkono juhudi za maendeleo hususan katika nyanja ya elimu".Amesema.

“Hivyo naomba wazazi waendelee kuleta watoto wao hapa ambapo kutokana na mradi wa elimu bure, vijana wao watapata mafunzo bila malipo ingawa wao watakacholipia ni shilingi 50,000 tu kwa ajili ya mtihani wa mwisho unaosimamiwa na mamlaka nyingine za elimu,” amesema.

Pia Dkt, Msuya ametanabaisha kuwa wapo katika mchakato kutoa ufadhili wa masomo ‘Scholarship’ kwa wanafunzi ambao wamepita na walipo katika chuo hicho kwenda kuongeza elimu zaidi nje ya nchi kwa aliyefikisha vigezo ikiwemo kupata alama za masomo zinazohitajika.

Ameongeza kuwa kinachotakiwa ni wanafunzi kuongeza juhudi ya kufanya vizuri katika masomo yao ili Shirika la Furaha lenye makao yake makuu jijini Dodoma,litakapoleta nafasi hizo za masomo nje ya nchi ziwakute vijana wenye vigezo wakiwa tayari wakisubiri muda tu.

Sambamba na hayo  Dkt Msuya amesema kuwa wapo katika mkakato wa kuanza kutoa mafunzo ya uuguzi ya mwaka mmoja lengo likiwa kuisadia serikali katika sekta ya afya kwani  wanafunzi watakaohitimu wataenda kufanya kazi ya kujitokea katika Hospitali za Serikali, huku Shirika la Furahika litakuwa likiwahudumia kwa posho, malazi na chakula kwa kipindi chote watakachokuwa wakitoa huduma hiyo.

“Tumeshatuma maomba Serikalini ili kuanza kutoa mafunzo hayo ya uuguzi bure na pindi tutakapokubaliwa mchakato huo utaanza haraka kwa kuanza usaili wanafunzi wa kozi hiyo ila kwa sasa tunaendelea na usaili wa wanafunzi wa kozi ya Ushonaji, Hoteli, Compyuta, IT, Udereva, Umeme,Bandari na mwisho wa kupokea maombi ni Julai 3, mwaka huu.

“Tunatoa wito kwa wazazi kuchangamkia fursa  hiyo kwa kuwaleta vijana wao kupata elimu bure kwa kozi wanazotaka ili kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika nyanja ya elimu kwa kufanikisha ndoto za watoto ambao wamekosa fursa ya kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali za kimaisha,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad