Mradi
wa Kongani ya kisasa ya viwanda Modern Industrial Park ,Disunyara
,Mlandizi Kibaha, Mkoani Pwani (KAMAKA) inayojenga viwanda 202 katika
eneo la ukubwa wa ekari 1077 imefikia asilimia 93 katika awamu ya kwanza
ya ujenzi wa miundombinu ambao utakamilika mwezi Februari mwaka 2024.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji(Mb.)
Januari 09,2024 alipotembelea eneo la Mradi huo katika eneo la
Disunyara/Kikongo, Mlandizi wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kujionea
utekelezaji unavyoendelea na kuona changamoto zilizopo ili kuzibeba na
kwenda kuzifanyia kazi kupitia Mawaziri wa kisekta.
Alisema
Tanzania iliamua isiachwe nyuma na mapinduzi ya nne na kuelekeza nguvu
katika maendeleo ya viwanda ili kujenga nchi katika nyanja mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa
inayoishia mwaka 2025 ambayo imeelekeza kuwe na viwanda
“Tumeunganisha
jitihada kuhakikisha malengo yanatimia na tunampongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kwa utayari wake ulioonesha kuwa ujenzi wa uchumi nchi upo
mikononi mwa sekta binafsi,” alisema Dkt. Kijaji na kuongeza kuwa
mwekezaji wa Mradi huo ni KAMAKA COMPANY LIMITED wa Dar es Salaam
akishirikiana na Serikali ya Tanzania.
Alisema kupitia uwekezaji
huo malengo ya vijana milioni moja wanaohitimu katika vyuo mbalimbali
wanaweza kufikiwa kwa ajira na Serikali iko tayari kushirikiana ili
malengo ya uwekezaji huo yaweze kufanikiwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Abubakar Kunenge alieleza kuwa barabara ya kuanzia Makofia
-Mlandizi -Mzenga -Vikumburu -Mloka ni muhimu kwani inapitia eneo la
uwekezaji na miradi ya kimkakati na kuomba ujenzi huo ukianza uanzie
Mlandizi kwa maslahi mapana ya eneo hilo.
Akisoma taarifa ya
Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Afriq Engineering and Construction
Company Limited Mhandisi Charles Bilinga alisema makadirio ya awali
yanaonesha kuwa ajira zisizopungua 200,000 zitatokana na mradi huo
ulioanza Oktoba 2021 kwa wakazi wa maeneo ya jirani na kongani ambapo
ajira za moja kwa moja zinakadiriwa kuwa 30,000 na pato la Serikali
litaongezeka kupitia Kodi mbalimbali
Mhandisi Bilinga alisema
gharama za mradi huo hadi kukamilika ni sh trilioni 3 na bilioni 500 na
kati ya fedha hizo sh bilioni 122 na milioni 400 zitatumika kujenga
miundombinu yote ndani ya kipindi cha miaka mitano nahadi sasa kiasi cha
sh bilioni 35 zimetukima kwa ujenzi w amiundombinu.
Kwa upande
wake Ofisa Fedha na Masoko wa Turnkey Real Estate wauzaji wa viwanja
kwenye mradi huo Bw. Tumaini Kabengula alisema mpaka sasa kuna mikataba
10 ya ununuzi wa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa viwanda,kuna viwanja 24
vilivyoshikiliwa vikisubiri kusainiwa kwa mkataba, wawekezaji watatu
wamekwishaanza hatua za awali za ujenzi na wengine watano waliosaini
mikataba wataanza mwaka huu.
Alisema wawekezaji waliotembelea
kongani kwa nia ya kuwekeza ni 58 wakitokea India China, Urutuki, Sudan
ya Kusini, Afrika Kusini, Rwanda, Somalia, Tanzania, Pakistan, Yemeni,
Zambia, Falme za Kiarabu, Misri, Uganda, Kenya na Canada.
Mradi
huo ulianza kutekelezwa oktoba 2021 ,kwa awamu ya kwanza kwenye ujenzi
wa lango kuu na uzio, kituo cha polisi, jengo la utawala, ofisi na jengo
la makazi ya wafanyakazi wa zimamoto, zahanati, kituo cha umeme wa
megawati 54 , mfumo wa barabara za nje na ndani na umefikia asilimia 93"
alibainisha Mhandisi Charles Bilinga.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea eneo la mradi wa Kongani ya kisasa ya viwanda iliyopo katika eneo la Disunyara na Kikongo Mlandizi Kibaha pwani jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya Afriq, Mhandisi Charles Bilingi (wa pili kulia) na maofisa wengine


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)




.jpeg)





No comments:
Post a Comment