Na Mwandishi Wetu,
MBUNGE
wa jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa
kwa kushirikiana na Oryx Gas Tanzania amegawa mitungi gesi 900 yakiwa
na majiko yake kwa Mama Lishe wote wa Wilaya ya Rufiji, lengo likiwa
kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Ugawaji huo wa
mitungi ya gesi ya Oryx umefanya wakati tayari Rais Dk.Samia Suluhu
Hassan amezindua Mpango wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa
Wanawake wa Bara la Afrika.
Akizungumza wakati wa kugawa mitungi
hiyo kwenye Wiki ya kukumbuka mchango wa Bibi Titi Mohamed ambaye enzi
za uhai wake ametoa mchango mkubwa katika kulikomboa Taifa hili ambapo
Waziri Mchengerwa na Oryx wameona iko haja kuwakumbuka Mama Lishe wa
Rufiji kwa kutambua mchango wao katika kuinua uchumi wao na Taifa kwa
ujumla sambamba na utunzaji mazingira.
Wakati anazungumza
Mchengerwa amesema matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa yakichangia
uharibifu wa mazingira na kusababisha kero mbalimbali nchni, hivyo
kutumia nishati safi ya kupikia kutapunguza uharibu wa maazingira lakini
pia kulinda afya za wanawake na watoto ambao ndio waathitika wakubwa wa
moshi wa kuni wakati wa kupika.
"Tunatambua mchango mkubwa wa
kundi hili la mama zetua na dada zetu ambao wanajihusisha na shughuli za
Mama Lishe, hivyo kwa kushirkiana na viongozi wenzangu wakiwemo
madiwani tulikubabaliana tutafute mitungi ya gesi ya orxy na kisha
kuwapatia mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji ambao idadi yao ni 1300 .
"Hivyo
leo kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx tunagawa bure mitungi 900
yakiwa na majiko yake bure na mitungi iliyobakia tutagwa hivi
karibuni.Tunataka kuona Mama Lishe wa wilaya ya Rufiji wanakuwa sehemu
ya kutunza mazingira kwa kupikia nishati safi...
"Lakini wakati
huo huo kuwalinda dhidi ya athari zinazotokana na kuvuta moshi wa kuni
wakiwa katika shughuli zao za kila siku,”amesema Mchengerwa huku
akisisitiza umefika wakati wa wananchi kuungana na Serikali
inayoongozwa na Rais Samia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya
kupikia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas
Tanzania Benoit Araman amesema wamefurahi kupeleka nishati safi ya
kupikia kwa wananchi wa wilaya ya Rufiji na kugusa kundi hilo muhimu
katika jamii ambalo shughuli zao za kila siku zinahitahi kupata nishati
ya kupikia.
“Kupika katika gesi ya oryx ni kulinda mazingira kwa
kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na
watoto ambao wamekuwa wakiathirika kwa kuvuta moshi mbaya unaotokana na
kuni. Rais wetu Mama Samia amejipanga kuhakikisha wananchi wote nchini
wanapata nishati safi ya kupikia ifkapo 2032.
“Katika mkutano wa
Dubai ,Rais Samia amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa
wanawake wa Afrika.Oryx Gas tutaendelea kushirikiana na Serikali ya
Tanzania kuhamasisha matumizi ya nishati safi ua kupikia kwa kugawa bure
mitungi ya gesi na majiko yake.
“Hadi leo hii Oryx tunajivunia
kwa kutoa mitungi zaidi ya 15000 yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni
moja katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa kupitia mpango
wetu wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kuungana
na Rais Samia katika kuhamaisha wananchi kutumia nishati hiyo.Ahadi yetu
kwa Serikali tutaendelea kuhamasisha kwa kugawa bure mitungi na majiko
kwa makundi mbalinbali ya wananchi.
Akieleza zaidi amesema
kutumia nishati safi ya kupikia kunafaida kubwa za kiafya na kimazingira
lakini wakati huo huo inatoa nafasi kubwa ya watoto kupata nafasi ya
kwenda shule kupata elimu badala ya kutumia muda mwingi kwenda kukusanya
kuni.
”Nakushukuru Waziri Mchengerwa kwa kufanikisha mpango huu
wa nishati safi ya kupikia kwa wnanchi wa Rufiji kwa kuwapatia mitungi
ya gesi 900."
Awali Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa
wa Pwani, Jenipher Shirima ameeleza kwa kina namna ambavyo vimetungi ya
gesi inaweza kutumika kwa usalama bila kuleta athari.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman ( katikati) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania( UWT) Marry Chatanda( wa pili kulia), Katibu Mkuu wa UWT Jokate Mwegelo(wa tatu kulia) , Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa(wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa Oryx na jiko lake mmoja wa Mama Lishe wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani( wa tatu kushoto), lengo ni kuwawezesha Mama Lishe kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kuni na mkaa.Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa Oryx Peter Ndomba na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa Pwani Zainab Vullu.Jumla ya mitungi 900 ya Oryx Gas na majiko yake yametolewa bure kwa Mama Lishe wote wa Wilaya hiyo
No comments:
Post a Comment