JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


GAVU AUNGANA NA BARAZA LA WAZEE MKOA WA TANGA KUWAOMBEA DUA NA KUTOA POLE KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG MKOANI MANYARA

Share This


Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndg. Issa Gavu amekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Baraza la wazee Mkoa wa Tanga uliohudhuriwa na wajumbe wa Baraza la wazee wilaya zote tisa Mkoani Tanga na kuwaombea Dua na kuwapa pole waathirika wa mafuriko wilaya ya Hanang na majeruhi wapone haraka.

Ndg. Issa Gavu baada ya Dua hiyo amewasikiliza wazee wa Mkoa wa Tanga na kupokea Maoni,Ushauri na Hekima ya namna ya kuendelea kuongoza wananchi waliokiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kukipa nafasi ya kuiongoza Serikali.


Aidha Ndg Gavu ameeleza madhumuni ya kuanzishwa kwa kanuni ya Baraza la wazee ya 2019 ni pamoja na :-

1. Kurithisha kwa Taifa Busara,Hekima na Ujasiri wao ndani ya Jamii.

2. Kuendelea kuwa Mfano bora wa Tabia njema kwa Taifa na hivyo kuongoza mafanikio ya Imani, Malengo na Madhumuni ya Chama Cha Mapinduzi.

3. Kushauri viongozi wa CCM ngazi zote kwa Hekima kuhusu njia bora za Ujenzi wa CCM na Taifa.

4. Kuona kwamba Nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya kudumisha Amani, Demokrasia,Utulivu na Uongozi bora.

5. Kuhifadhi, Kukuza na kudumisha Umoja na Uzalendo wa kitaifa.

6. Kuwaunganisha wazee wote wa CCM katika Imani na mwelekeo wa kiitikadi wa CCM.

“Hivyo basi wazee mkirudi katika maeneo yenu mkashauri mkiwataka viongozi wa CCM wenyeviti wa vijiji na vitongoji na mitaa kusoma mapato na matumizi pamoja na kusimamia maadili ya Chama Cha Mapinduzi.” Amesema Ndg Issa Gavu.

Ndg. Issa Gavu ameendelea kukiri Chama Cha Mapinduzi kipo mikononi salama kwa wazee na waasisi wa Chama Cha Mapinduz.

Wazee wa Mkoa wa Tanga wamempongeza Mwenyeketi wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuwasikiliza, kuchota Busara na Ushauri kutoka katika Kundi hili la Wazee

Ndg Gavu ameyasema hayo akiwa katika ziara ya Mkoa kwa Mkoa akisikiliza Busara, Ushauri na Hekima za Baraza la wazee wa Mkoa husika namna ya kuimarisha na kukiendeleza Chama Cha Mapinduzi pamoja na Ushindi wa kishindo katika Chaguzi za serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 .


#KaziIendelee

#TangaKunani

#IsiyokongweHaivushi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad