JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Betpawa yatangaza washindi 20 wa awamu ya pili wa kampeni ya Dream Maker.

Share This
Tunapokwenda kuwatangaza washindi wa awamu ya pili nichukue nafasi hii pia kuwakumbusha kuwa kampeni hii ilianza mwa 2021 na betpawa iliwashika mkono vijana wakitanzania 13 kwakuwezesha nakufanikisha ndoto zao ambapo waliweza kujenga nyumba,viwanja vya michezo pamoja na kuanzisha Biashara.

Pia Dream Maker imeweza kufanya ukarabati wa kituo cha afya pamoja na mradi wa maji, mradi wa kwenda masokoni kwa majiko sanifu ambayo ni Rafiki kwa mazingira na mingine ya kijamii na kibiashara inayolenga kuboresha Maisha ya wanufaika mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla,” alisema Meneja masoko wa BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu.

Kampeni hiyo iliyokuwa wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, ilifanyika kupitia basi maalum lililojulikana kama Dream Bus ambapo wakazi wa Lindi, Mtwara na Ruvuma walipewa fursa ya kupanda kwenye basi na kuelezea ndoto au mawazo yao ya miradi zoezi ambalo lilifanyika mwezi mmoja uliopita.

 Maombi mengine yalitumwa kwa njia ya mtandao kupitia video kupitia kurasa za mitanado ya kijamii kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker Akiwatambulisha washindi 20 wa msimu huu wa pili wa BetPawa DreamMaker jijini Dar es Salaam leo, Borah alisema kuwa miradi hiyo 20 bunifu ilitokana na mamia ya ndoto na mawazo mbali mbali ya miradi kutoka kwa washiriki tofauti iliyokusanywa kupitia kampeni ya Basi la Ndoto (Dream Bus), na kwenye tovuti na mitandao ya kijamii.“Dream Bus ilizunguka nchini mwezi Oktoba, huku watu wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wakialikwa kuingia ndani ya basi na kueleza ndoto zao.

Wengine wengi walishiriki mtandaoni kupitia #betPawaDreamMaker na kwa kutuma video, na BetPawa ilipitia kila ndoto kabla ya kuchagua ndoto 20 bora za kusaidia na kuzifanya kuwa kweli” aliongeza.DreamMaker inamwezesha Anania Muba kutoa huduma bora na salama zaidi za afya katika zahanati ya Nangomba .


Anania ana ndoto ya kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati hiyo, akifafanua kuwa jengo linalotumika sasa limeharibika na si salama kwa ajili ya kutoa huduma za afya. “Nawashukuru BetPawa kwa kukubali kutimiza ndoto yangu ya kuchangia ujenzi huu utakaoboresha maisha ya mamia ya wakaazi wa eneo hili wanaotegemea kliniki hii kwa ajili ya huduma zao za afya,” alisema.

Kwa upande wake mshindi wa kampeni hiyo Herman Mwakatobe mkazi wa Mbeya sasa anajiandaa kufungua kiwanda kinachotengeneza majiko rafiki kwa mazingira yanayotumia mafuta yaliyotumika ya vilainishi/ oili chafu kama nishati mbadala ya kupikia. Anatarajia kuwa majiko hayo yatatumika nyumbani, migahawani, shuleni, vyuoni, na katika viwanda vya sabuni, ili kulinda mazingira kwa kupunguza ukataji miti na kutumia nishati hiyo mbadala" Nikifanikiwa kutimiza ndoto yangu, nitatoa ajira kwa jamii katika kiwanda changu na sokoni, na nitaita jiko hilo Pawa,”

Mwakatobe alisema.BetPawa pia itamwezesha Eric Salema kushughulikia tatizo la uhaba wa maji Sanya Juu, Kilimanjaro kwa kujenga kisima na kuvuta maji kutoka kwenye kisima hicho ili kusaidia wakulima na wafugaji wa jumuiya hiyo.

Nafurahi kuwa BetPawa watatuwezesha kupata maji ya uhakika ambayo yatatusaidia kulima mboga na kunywesha mifugo yetu, ili kuboresha maisha yetu wote," alibainisha.Washiriki wengine ambao ndoto zao zitatimia ni pamoja na Khadija Bundala wa Dar es Salaam atakayepata bajaji mpya kwa ajili ya biashara.

Makusanyo ya biashara yatamsaidia kumpeleka mwanae kupata huduma za afya za kila mwezi katika kliniki ya wagonjwa wa seli mundu (sickle cell), kulipia dawa anazotumia kila siku, pamoja na huduma za uhakika za chakula na ada ya shule. Vile vile, BetPawa DreamMaker itatimiza ndoto ya Delphinus Magezi ya kufungua karakana ya uhunzi, uchomeaji vyuma na kutengeneza vifaa vya aluminium pamoja na kutoa mafunzo kwa vijana 20 kila mwaka, ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana jijini Dodoma.

“Naye Samson Lazaro wa Kahama anayeota kuwa na studio ya kurekodi muziki, pamoja na Eric Kimena wa Dar es Salaam mwenye maono ya kumiliki studio ya video na picha wote sasa wapo karibu kupaa na kutimiza malengo yao kwa nguvu za BetPawa DreamMaker,” Borah alimalizia.

Dream Maker ya betPawa inaendelea kubainisha na kutimiza ndoto za Kitanzania zenye ushawishi kuwa kweli. Msimu uliopita wa kwanza wa BetPawa Dream Maker ulifanyika September 2021 na kubainisha ndoto za nyumba, biashara na huduma za michezo zinazoendelea kunufaisha maisha ya jamii na kuibua fursa mpya za biashara.

Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya betpawa Bi Borah Ndanyungu (katikati), akizungumza  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza washindi wapya wa awamu ya pili wa kampeni ya Dream Maker ilianzishwa mahususi kwaajili yakutimiza ndoto za watanzania. Wengine pichani ni washindi hao Anania Muba kushoto na Hermani Mwakatobe
Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya betpawa Bi Borah (kulia), pamoja na Msimamizi wa Masoko wa kampeni hiyo Nasoro Mungaya kushoto wakimsikiliza mmoja ya washindi 20 wa kampeni ya Dream Maker Ismail Kahanda wapili kushoto wakati wa hafla ya kutangaza washindi wapya wa awamu ya pili wa kampeni hiyo. Mwengine pichani ni Balozi wa Dream Maker David Kampista.
Washindi wapya wa awamu ya pili wa kampeni ya Dream Maker ya Betpawa wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad