Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ameonyesha kuvutiwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na benki ya
Exim Tanzania katika kujitanua na kusogeza huduma zake karibu zaidi kwa
wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hatua hiyo ameitaja kuwa
itasaidia kukuza uchumi wa maeneo husika na kuimarisha utangamano wa
kijamii.
Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo jana
alipotembelea banda la maonesho la Benki ya Exim Tanzania muda mfupi
kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha yanayoendelea
kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Benki ya Exim ni moja
ya wadau muhimu wa Maonesho hayo yanayotarajiwa kuhitimishwa Novemba 26,
mwaka huu.
Akiwa kwenye banda la benki ya Exim, Waziri Mkuu
alipata wasaa wa kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na
benki hiyo kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi
Kauthar D’Souza ambae pamoja na kuelezea baadhi ya huduma za kifedha
zinazotolewa na benki ya Exim Tanzania pia alielezea kuhusu mkakati wa
benki hiyo katika kujitanua katika maeneo mbalimbali nchini.
“Niwapongeze
sana kwa jitihada mnazoendelea kuzifanya katika kupanua zaidi huduma
zenu, hata hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili hizi huduma nzuri
mnazoendelea kuzitoa ziwafikie wananchi wengi zaidi hususani waliopo
pembezoni huko ambao bado hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha.’’
Alishauri Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa alitumia
fursa hiyo kutoa wito kwa watoa huduma za kifedha nchini kuhakikisha
wanaendelea kutoa elimu ya fedha kwa umma sambamba na kupunguza gharama
za uendeshaji wa huduma hizo zikiwemo riba na ada ili wananchi wengi
watumie huduma za fedha zilizo rasmi.
Awali akielezea kuhusu
huduma za benki ya Exim Tanzania mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa, Bi
Kauthar alisema licha ya jitihada za benki hiyo katika kujitanua zaidi
nchini ambapo hadi sasa ina mtandao wa matawi 33 na mawakala 1500 nchi
nzima, bado mkakati wake ni kuwekeza zaidi katika utoaji wa huduma
kupitia ubunifu wa kidijitali ili kutoa masuluhisho ya kibenki yanayofaa
na salama kwa wateja wake.
“Pia tunatambua wajibu tulionao
katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini na ndio
sababu moja ya kipaumbele chetu ni kuwawezesha watu binafsi na
wafanyabiashara wakiwemo wanawake na wajasiriamali kupitia huduma zetu
mahususi kwa ajili yao ikiwemo akauti ya Wajasiriamali pamoja na akaunti
ya ‘Supa woman’ iliyobuniwa kwa ajili ya wanawake wanaopambana kukuza
mitaji ya biashara zao," aliongeza.
Zaidi, Bi Kauthar alibainisha
kuwa benki ya Exim Tanzania imeendelea kujitolea kuinua jamii huku
akiutaja mpango wa Exim Cares wa benki hiyo kama nguzo muhimu katika
utekelezaji wa juhudi mbalimbali za benki hiyo katika kuchangia
maendeleo ya nchi kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR)
hususani katika sekta muhimu zikiwemo elimu, afya, michezo na utunzaji
wa mazingira (Exim Go Green Initiative). Katika kuthibitisha dhamira
hiyo benki ya Exim kupitia maonesho hayo imeambatana na baadhi ya
wajasiriamali wanawake ambao ni wanufaika na Programu ya Uwezeshaji
Wanawake (WEP) ya benki hiyo waliopata fursa ya kuonesha bidhaa zao
wakiwa kwenye banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye
Maadhimisho hayo.
“Kwa kufanya hivyo, sio tu kwamba tunatimiza
wajibu wetu kama benki lakini tumekuwa mawakala wa mabadiliko chanya
ndani ya jamii zetu,” alisisitiza.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili Kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa
wa benki ya Exim Tanzania akiwemo Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki
hiyo Bi Kauthar D’Souza (katikati) na Meneja wa Benki hiyo tawi la
Mt.Meru, Arusha Bw Eliud Massaga (wa tatu kushoto) pamoja na mofisa
wengine wa benki hiyo wakati alipotembelea banda la maonesho la benki ya
Exim muda mfupi kabla ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya
Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana. Kulia ni
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili Kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa
wa benki ya Exim Tanzania akiwemo Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki
hiyo Bi Kauthar D’Souza (wa pili kushoto) na Meneja wa Benki hiyo tawi
la Mt.Meru, Arusha Bw Eliud Massaga (kushoto) wakati alipotembelea banda
la maonesho la benki ya Exim muda mfupi kabla ya kufungua Maadhimisho
ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha jana.
Meneja
wa Benki ya Exim tawi la Mt.Meru, Arusha Bw Eliud Massaga (kushoto)
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba (katikati)
alipotembelea banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha jana. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki
hiyo Bi Kauthar D’Souza
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba (kushoto) akitazama baadhi ya bidhaa
zinazozalishwa na wajasiriamali wanawake ambao ni wanufaika na Programu
ya Uwezeshaji Wanawake (WEP) ya Benki ya Exim wakati alipotembelea banda
la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya
Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana.
Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bi
Kauthar D’Souza (wanne kulia) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mt.Meru,
Arusha Bw Eliud Massaga (wa tano kulia)
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba (wa pili kushoto) akizungumza na
baadhi ya wajasiriamali wanawake ambao ni wanufaika na Programu ya
Uwezeshaji Wanawake (WEP) ya Benki ya Exim wakati alipotembelea banda la
maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma
ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana..
Baadhi
ya wajasiriamali wanawake ambao ni wanufaika na Programu ya Uwezeshaji
Wanawake (WEP) ya Benki ya Exim akiwemo Bi Rahma Juma (Kushoto), Mariam
Mohamed (katikati) na Bi Rahel Nombo wakiwa tayari kuwahudumia wateja
wao kwenye banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye Maadhimisho
ya Wiki ya Huduma ya Fedha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha jana.
Waziri Mkuu Majaliwa Avutiwa na Jitihada za Benki ya Exim Kusogeza Huduma kwa Wananchi.
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.


No comments:
Post a Comment