Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa usimamizi thabiti wa sekta ya fedha nchini pamoja na jitihada inazofanya katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma za fedha.
Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo
alipotembea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha
Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
ambapo alipokelewa na Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya
Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo.
Bi. Msemo alisema kuwa katika
maadhimisho hayo BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu haki zao kutoka kwa
taasisi za fedha pamoja na wajibu wa wananchi katika kutumia huduma za
fedha.
Katika banda la Benki Kuu wananchi wanapata fursa
yakujifunza kuhusu sera za uchumi na fedha; uwekezaji katika dhamana za
serikali; usimamizi wa fedha binafsi, akiba, mkopo; namna BoT inawalinda
watumiaji wa huduma za fedha; utunzaji sahihi wa noti na utambuzi wa
alama za usalama; mifumo ya malipo ya taifa na namna Bodi ya Bima ya
Amana inavyokinga amana za wateja wa benki na taasisi za fedha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akipewa maelezo na Naibu Gavana, Bi. Sauda Kassim Msemo, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akipewa maelezo na Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akielezea jambo kwa Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses, alipotembelea banda la BoT kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


No comments:
Post a Comment