Tanzania Commercial Bank jana
iliungana na mataifa mbalimbali duniani kote kuadhimisha Wiki ya Huduma
kwa mteja kwa mwaka 2023 ilikuwa na kaulimbiu ya “TEAM SERVICE” hiyo
huku benki hiyo ikijikita zaidi na dhamira yake ya kuendelea kutoa
huduma bora na zinazokidhi mahitaji ya wateja.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki wa huduma kwa wateja Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo ambaye ni mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema
Msuya alisema benki ya TCB inachukulia kwa ukubwa wa hali ya juu sana
kutoa huduma kwa wateja ndiyo maana kwa Tanzania commercial bank huduma
ni moja ya mikakati na utamaduni wa benki hiyo.
Msuya
alisema “kaulimbiu ya mwaka huu inaendana hasa na utekelezaji wa
majukumu yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu wa Tanzania Commercial
Bank na kuboresha huduma ni hamasa ya biashara na TCB imeweka kipaumbele
cha kutoa huduma bora kwa wateja”.
"Hii
ndiyo sababu Tanzania Commercial Bank inaendelea kuwekeza mara kwa mara
katika jamii na kuwapa wafanyakazi wetu ujuzi na rasilimali
zinazohitajika ilikuhakikisha wanawapa wateja wetu huduma za hali ya
juu," Msuya alisema.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa
Tehama Bw. Jema Msuya akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya wiki
ya huduma kwa mteja. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi la Mlimani City
jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM
SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea
kutoahuduma bora kwa wateja wake.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa
Tehama Bw. Jema Msuya (katikati) akikata keki pamoja na wateja wa benki
hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja katika tawi la
Mlimani City jijini Da es Salaam. hivi karibuni ambapo ilikuwa na
kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki
yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa
Tehama Bw. Jema Msuya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
maafisa wa benki hiyo.jpeg)
Baadhi
ya maofisa wa Tanzania Commercial Bank pamoja na wateja wa benki hiyo
wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa
mteja.


No comments:
Post a Comment