Na Said Mwishehe,Michuzi TV
TUME
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imeelezwa kwamb sekta
binafsi nchini imekuwa na mchango mkubwa kuinua bunifu kwa kutoa mawazo
mazuri ya kuboresha sera.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam
wakati wa kutangaza kuanza kwa Maonesho ya Wiki ya Sahara Sparks
yanayotoa fursa wabunifu kuonesha bunifu zao Mkurugenzi Menejimenti
Maarifa Costech Samson Mwela ameeleza kwa kina mchango wa sekta binafsi
katika kuibua wabunifu.
Amesema Serikali imekuwa ikitenga fedha
na kuingiza kwenye sekta ya kuendeleza ubunifu na ili ziweze kuelekezwa
maeneo yenye manufaa na tija wanahitaji zaidi maoni ya wananchi na sekta
binafsi huku akisisitiza ili kuendeleza bunifu zinazoibuliwa iko haja
kwa wadau kuwa sehemu ya safari hiyo.
Amefafanua kwamba kwa muda
muda sekta binafsi ikiwemo ya Sahara Sparks zimekuwa zikiandaa maonesho
mbalimbali nchini ambapo wabunifu huonesha bunifu zao na zile zenye
tija zimekuwa zikiendelezwa .
"Sekta binafsi katika eneo hili la
ubunifu wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana, ziko bunifu nyingi ambazo
zimeleta manufaa makubwa na siwezi kuzitaja hapa maana wote tunafahamu.
"Lakini
sekta binafsi wamekuwa wanafanya mijadala ambayo imekuwa ikiibua mawazo
mazuri yanayokusanywa na Serikali kabla ya kuyachakata na yamekuwa
msaada kufanikisha utungaji sera na kuchochea mageuzi ya tasnia ya
bunifu nchini na tuko katika mchakato wa kuangalia upya sera zetu kwa
lengo la kuendelea kuboresha eneo hili la ubunifu,”amesema
Akifafanua
zaidi amesema mawazo hayo mazuri yamekuwa yakiingizwa kwenye program
zao na kusisitiza kupitia program zilizoanzishwa kuanzia mwaka jana,
jumla ya vijana 83 wamenufaika na mfuko wa kuendeleza bunifu za vijana.
Ameongeza kwamba kati yao vijana 150 wanaotarajia kwenda kushiriki maonesho ya Sahara wameptia kwenye tume hiyo.
Awali
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Venture, Mussa Kamata amesema kampuni
hiyo tangu mwaka tangu mwaka 2016 wamekuwa wakifanya maonesho ya
ubunifu na wanajivunia mafanikio yaliyopatikana yakiwemo kuwawezesha
vijana 2000 kupata fursa hiyo kuonesha bunifu zao.
Amesisitiza
kuwa kati yao kuna walionufaika kupata msaada wa kifedha, kutoka kwa
wawekezaji ambao ni zaidi ya vijana 12 kupitia jukwaa hilo na sasa
wanaendeleza bunifu zao.
"Tuliamua kuanzisha kuanzisha jukwaa kwa
lengo kuu la kuwasaidia vijana wabunifu nchini kuwa na eneo ambalo
wataonesha bunifu zao na kutoa maoni yao katika eneo la ubunifu."
Wakati
huo huo Meneja wa Sahara Sperks Lead Rose Urassa amefafanua kuhusu
maonesho hayo huwa yanafanyika kila mwaka kwa ajili ya kunyanyua jukwaa
la sayansi na teknolojia nchini kupitia ubunifu na uwekezaji.
“Tukio
hili litafanyika kwa wiki nzima katika viwanda vya makumbusho ya Taifa
Posta na wabunifu mbalimbali watakuwa wanaonesha bunifu zao na kutakuwa
na wawekezaji watakao hudhuria kuona namna ya kuwaunga mkono,”amesema
Ameongeza
kutakuwa na matukio yanayoendelea kuanzia kesho na kuendelea mpaka
Oktoba 13, 2023 na maonesho yenyewe yatafanyika Oktoba 13 na Oktoba 14
katika viwanja vya Makumbusho vilivyopo Posta jijini Dar es Salaam .
"Oktoba
13 maonesho yataanza saa 11 jioni kwa wageni kuanza kuingia na
litaendelea mpaka saa nne usiku na siku ya pili ambayo ni Oktoba 14
tutaanza maonesho kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa nne usiku katika
eneo hilo hilo .
"Lakini kabla ya kufika Oktoba 13 , kuanzia
kesho Oktoba 10 kutakuwa na matukio mengine yanaendelea kuelekea katika
kilele chenyewe cha Sahara, " amefafanua.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Venture Mussa Kamata( kulia) akifafanua kwa kina kuhusu maonesho ya ubunifu ya Sahara Sparks yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam .Katikati ni Mkurugenzi Menejiment maarifa kutoka COSTECH Samson Mwela na kushoto ni Meneja wa Sahara Sparks Rose Urassa

.jpeg)


No comments:
Post a Comment