NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa
na Michezo Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' anatarajiwa kufungua maonesho ya
sanaa za ubunifu nyumbani Tanzania, maonesho yatakayowahusisha wabunifu
mbalimbali wa Sanaa zikihusisha ujenzi, utengenezaji samani na usanifu
majengo ambayo yatafanyika kuanzia Agosti 25 hadi 27 mwaka huu katika
viwanja vya Warehouse Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mmoja ya wakurugenzi wa
kampuni ya Art & Home na waandaaji wa wiki ya Art & Home
Ameniel Lukumay amesema, maonesho hayo yatawakutanisha pamoja wabunifu
wa masuala ya nyumbani ambayo pia ni fursa kwa watanzania kupendezesha
nyumba zao kupitia wabunifu hao wazawa.
"Kuna wabunifu wengi wapo
mtaani, wanafanya kazi nzuri lakini ni ngumu kuwapata, Art & Home
tunawakutanisha wabunifu hawa na walaji ni wiki ya ubunifu na
kupendezesha nyumba kwa samani, kuziba nyufa na nakshi mbalimbali
zinazotokana na wabunifu wa hapa nyumbani..... watakuwepo wajenzi,
wataalam wa landscaping, interior and exterior designers." Amesema.
Amesema,
Sanaa ya ufundi inaonekana kusahaulika na wakaona kupitia wiki ya Art
& Home ni vyema kuwakutanisha wanasanaa ya ufundi na walaji pamoja
na kuwa na wiki ya kuzingatia masuala ya nyumbani ikiwemo kupanda miti,
maua na kubadilisha samani.
Pia Rais wa Shirikisho la Sanaa za
Ufundi Tanzania (TAFCA,) Adrian Nyangamalle amesema, zaidi ya watanzania
milioni nne wanajihusisha na sanaa za ufundi ambayo pia inachangia pato
la Taifa pamoja na kutoa ajira.
"Changamoto zinazoikabili sekta
hii ni soko, uwepo wa wiki ya Art & Home utasaidia sana wabunifu
kupata masoko na kubadilishana uzoefu...pia wananchi watapata fursa ya
kuona na kupata bidhaa zenye viwango kutoka kwa wabunifu wa hapa
nyumbani." Amesema.
Aidha amewahimiza watanzania kupenda bidhaa
zinazozalishwa nyumbani na kuwataka wabunifu kutumia fursa hiyo kwa
kujitokeza kwa wingi na kuonesha bunifu zao.
" Maonesho haya
yatazinduliwa tarehe 25 mwezi huu ambayo ni siku ya sanaa duniani,
mabanda yapatayo 100 yaliyoandaliwa yajae na nitoe wito kwa kampuni
mbalimbali zijitokeze kudhamini maonesho haya ambayo yamelenga kukuza na
kutangaza bunifu za sanaa ya ufundi hapa nchini." Ameeleza.
Aidha
Msemaji na Mhamasishaji wa maonesho hayo Japhet Ole amesema, wabunifu
mbalimbali wakiwemo wasanifu majengo na wajenzi watakutana pamoja walaji
pamoja na wabunifu hao kukutana kubadilishana ujuzi na uzoefu.
Aidha
amesema, viongozi na wadau mbalimbali wa fani hiyo watashiriki maonesho
hayo na kujadili namna ya kuiendeleza zaidi Sanaa ya ufundi.
Kwa
upande wake Meneja mauzo wa Art & Home Week Doris Lyimo amesema
kuwa maonesho hayo hayana kiingilio na wabunifu wakiwemo wajenzi na
wasanifu majengo wataonesha bidhaa zao na kuwahimiza kuendelea kupata
mabanda ya maonesho kupitia 0717664472.
Bi. Doris amesema
washiriki wote wa maonesho hayo watapata vyeti vya ushiriki pamoja na
tuzo kwa bunifu na waoneshaji bora katika maonesho hayo ambayo washiriki
kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar watashiriki huku mpango wa
kushirikisha nchi nyingine katika maonesho ya mwaka ujao ukielezwa.
Msemaji na Mhamasishaji wa maonesho hayo Japhet Ole (kushoto,) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maonesho hayo na kueleza kuwa viongozi mbalimbali na watu mashuhuri watashiriki maonesho hayo. Leo jijini Dar es Salaam.
Mmoja
ya Wakurugenzi wa Kampuni na waandaaji wa wiki ya Art & Home
Ameniel Lukumay (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea
mkutano huo na kueleza kuwa maonesho hayo yatawakutanisha wabunifu hao
pamoja na walaji na kuwa na wiki ya kuzingatia masuala ya ubunifu wa
nyumbani, Leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa bidhaa wa kampuni
hiyo na anayefuatia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania
(TAFCA,)Adrian Nyangamalle. Leo jijini Dar es Salaam.
Meneja mauzo wa kampuni ya Art & Home Bi. Doris Lyimo (kushoto,) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maonesho hayo na kutoa mwito kwa kampuni mbalimbali kujitokeza na kudhamini maonesho hayo. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.
No comments:
Post a Comment