Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA) imesema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kufikia malengo yake kwa kuhakikisha jamii inalindwa afya zao na inakuwa
salama kutokana matumizi ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa
nyinginezo zinazohusiana na afya.
Akizungumza leo wakati wa
Kikao kazi cha Wahariri na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka hiyo Adan Fimbo amesema katika kipindi cha miongo miwili katika
usimamizi wa bidhaa za dawa, vifaa tibana na vitendanishi wanajivunia
mafanikio makubwa katika kutoa huduma.
Ametaja baadhi ya
mafanikio yaliyokiwa katika kipindi cha miaka 20, ni kuanzishwa kwa
Mamlaka ya udhibiti, Kukamilisha ujenzi wa upanuzi wa Maabara ya Dar es
Salaam, Kubuni, kuanzisha na kutekeleza mradi wa Duka la Dawa Muhimu
(DLDM / ADDO)
Pia kuzindua na kuanzisha Ofisi ya Kanda ya Ziwa,
jijini Mwanza (sasa Kanda ya Ziwa Mashariki), kukamilisha ujenzi wa
Ofisi ya Makao Makuu ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa - TFDA
(sasa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu TMDA na Kanda ya Mashariki)
Ametaja mafanikio mengine ni kuzindua rasmi jengo la Ofisi ya Makao
Makuu ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa - TFDA (sasa Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu TMDA na Kanda ya Mashariki), kuanzisha, kukidhi na
kutekeleza mifumo ya utendaji kazi ya kimataifa ya ISO 1901:2018
Pia
kupata tuzo ya kuwa taasisi ya kwanza yenye mifumo bora ya utendaji
kazi Serikalini (Best Managed Institution in Tanzania), Maabara ya TMDA
kuwa na umahiri unaotambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO
Prequlified Laboratory) na Kituo cha umahiri wa usajili dawa barani
Afrika
Ametaja pia Maabara ya mafunzo ya umahiri kwa Mamlaka za
Udhibiti Dawa barani Afrika, Kuanzisha mifumo ya kielekroniki ya utoaji
huduma kwa wateja,Kutoa huduma za udhibiti kwa njia ya kielektroniki
(automation of regulatory services)
Fimbo ametaja kuimarika kwa
makusanyo hivyo kuchangia asilimia 15 ya mapato yake katika gawio la
Serikali na kuwa na ziada ya asilimia 70 kama inavyoekekezwa na Hazina
Mengine
ni Kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi ya TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki
Mwanza na kuanza kutumi, Kuanzisha mazingira wezeshi na rafiki ya
ufanyaji biashar nchini kwa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA
Pia
Kufikia Ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani - WHO(WHO Maturity L-3)
kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti dawa barani Afrika hivyo kuwa
taasisi ya kwanza ya udhibiti na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza
barani Afrika kufikia ngazi hiyo
Aidha Maabara ya TMDA kupata
hadhi ya juu ya ngazi ya nne umahiri wa Shirika la Afya D\uniani,
Kubadili jina kutoka TFDA kuwa TMDA, Kukamilisha ujenzi wa jengo la
Ofisi ya TMDA Kanda ya Kati Dodoma na kuanza kutumika
Pia Mamlaka
kupewa jukumu la udhibiti wa bidhaa za tumbaku,kuanzisha mfumo wa
kufuatilia utoaji taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa
njia ya simu
Mafanikio mengine ni Mamlaka kupata Hati safi kwa
miaka 20 mfululizo kutokana na ukaguzi wa hesabu za taasisi kwa ukaguzi
unaofanywa na ofisi ya CAG na kutimiza miaka 20 ya taasisi katika
kulinda afya ya jamii kwa ufanisi.
Akifafanua pamoja na
mafanikio tajwa, Mamlaka inaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzingatia
maoni ya wateja. mathalan, kwa Mujibu wa utafiti uuliofanywa na Shule
ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam
Business School) wa Desemba 2020 kuhusu wateja kuridhika na huduma
zitolewazo na Mamlaka.
Amesema katika halmashauri 28 kwenye mikoa
14 ya Tanzania, ulibaini kuwa asilimia 47 tu ya wananchi ndiyo
wanaifahamu TMDA. Ni dhahiri kwamba matokeo haya yanaakisi mabadiliko ya
jina la taasisi yaliyofanyika mwaka 2019.
"Hata hivyo, Mamlaka
inatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuongeza uelewa wa
wananchi kuifahamu Mamlaka.Kwa kuwa upo umuhimu mkubwa wa wadau wote wa
TMDA kuifahamu Mamlaka na majukumu yake...
"Wahariri na Waandishi
wa Habari wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa Mamlaka
inajulikana kwa jamii na Sheria tajwa inasimamiwa kiufanisi, TMDA
imekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau wake kwa lengo la kuwaelimisha
juu ya kazi zake sanjari na majukumu ya kila mdau katika kutekeleza
Sheria husika."
Kuhusu suala la uelimishaji jamii limepewa
kipaumbele kikubwa na TMDA na ndiyo sababu tumewaita hapa Wahariri
walioko mbele yako kwa lengo la kuwashirikisha mafanikio yaliyofikiwa na
TMDA ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kushirikiana zaidi katika
kuhakikisha kuwa soko la Tanzania lina bidhaa zilizo bora, salama na
fanisi ili kumlinda mlaji.
Amesema kimsingi, kazi hii sio rahisi
na inahitaji ushirikiano wa karibu kati yetu sisi TMDA, waandishi wa
habari na wananchi wote kwa ujumla wao.
Ameongeza ni matumaini
yao kupitia tasnia ya habari, wataweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na
kuwapa elimu endelevu ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa
kuchagua, kununua na kutumia bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA kutoka
katika soko.
Kuhusu Kikao kazi hicho amesema mada mbalimbali
zimewasilishwa katika kikao hiki ambapo ni matarajio yao kuwa baada ya
semina hiyo, washiriki waweze kuelewa vyema nini Mamalaka imetekeleza na
katika kuhakikisha sheria na majukumu ya TMDA yanatekelezwa katika
kulinda afya ya jamii.
Aidha, kupitia hoja zitakazoibuliwa baada
ya mada husika kutolewa, tutaainisha kwa pamoja maeneo ya ushirikiano
katika kuielimisha zaidi jamii kupitia vyombo vya habari kuhusu masuala
yahusuyo udhibiti wa bidhaa za dawa vifaa tiba na vitendanishi kutokana
na ukweli usimamizi wa Sheria hautakuwa na mafanikio kama hatutakuwepo
na ushirikishwaji wa wadau wetu hususan vyombo vya habari.
"Ni
imani yetu kuwa Wahariri na Waandishi hawa wakirudi kwenye maeneo yao ya
kazi wataweza kueneza ujumbe watakaopata leo kwa watu wengi zaidi na
hivyo kuwezesha jamii kupata elimu, kujilinda na kutumia dawa, vifaa
tiba na vitendanishi vilivyosajiliwa au kupitishwa na TMDA."
Mkurugenzi
Mkuu wa TMDA Adam Fimbo akizungumza wakati wa Kikao kazi cha Wahariri
na Waandishi wa habari kilichofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya Wahariri wa Habari na watendaji wa TMDA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam, albert Chalamila alipokuwa akizungumza katika kikao
kazi hicho.
Meneja
Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)
Gaudencia Simwanza akitoa neno la ukaribisho kwa Wahariri wa Habari
waliohudhuria katika kikao kazi hicho.
Baadhi ya Wahariri wa Habari na Watendaji wa TMDA katika kikao kazi hicho.
Picha ya Pamoja. Kaimu
Meneja Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Martha
Malle, akitoa mada katika kikao kazi hicho kuhusu Sheria na Kanuni
mbalimbali za udhibiti, za Mamlaka hiyo.
TMDA YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE KATIKA KIPINDI CHA MIONGO MIWILI
Share This
Tags
# HABARI
Share This
Jiachie Blog
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
A Tanzanian blog operating since 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.
No comments:
Post a Comment