BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake ya kufanikisha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Afrika kusini kwa kuwawezesha wafanyabiashara wa mataifa hayo mawili ili waweze kupanua zaidi biashara zao sambamba na kuchangamkia fursa zaidi nje ya mipaka ya nchi hizo kufuatia hatua ya Umoja wa Africa kujumuishwa kuwa mwanachama wa kudumu katika muungano wa Umoja wa bara Ulaya G-20.
Dhamira hiyo imewekwa bayana na
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa Benki ya NBC Bw Peter
Nalitolela wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
hiyo Bw Theobald Sabi kwenye Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa
Afrika Kusini nchini Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam jana
jioni ukihudhuriwa pia Balozi wa Afrika Kusini hapa Tanzania Bi
Noluthando Malepe.
Kwa mujibu wa Bw Nalitolela, kupitia huduma
zake mbalimbali za kifedha ikiwemo mikopo ya ukuzaji mitaji, dhamana,
huduma ya fedha za kigeni sambamba na huduma ya malipo kwa njia ya
mtandao inayofahamika kama ‘NBC Connect’ benki hiyo imedhamiria
kurahisisha zaidi ufanisi wa biashara kwa wafanyabiashara wa mataifa
hayo ili waweze kushiriki kwa ushindani zaidi kwenye fursa hiyo mpya ya
kimataifa.
“Tumefurahi kuona kwamba Mheshimiwa Balozi wa Afrika
Kusini hapa Tanzania Bi Noluthando Malepe nae amewasisitiza
wafanyabiashara kuchangamkia soko hili jipya la G -20 nasi NBC pia
tunawathibitishia kuwa tupo tayari Kwenda nao bega kwa bega kufanikisha
hili kupitia huduma zetu muhimu za kifedha ambazo zimebuniwa mahususi
kurahisha mahitaji yao ikiwemo mikopo, dhamana, upatikanaji wa fedha za
kigeni na zaidi huduma yetu ya malipo kwa njia ya mtandano yaani NBC
Connect itakayowawezesha kufanya mihamala mbalimbali yakiwemo malipo ya
serikali na tozo mbalimbali’’ alitaja.
Alisema kwa muda mrefu
sasa benki hiyo imekuwa mdau mkubwa wa wafanyabiashara kati ya Afrika
Kusini na Tanzania ambapo kupitia mkutano huo uliodhaminiwa na benki ya
NBC, alitaja baadhi ya sekta zinazotazamwa zaidi na benki hiyo kuwa ni
pamoja na sekta za kilimo, usafirishaji, mawasiliano, biashara na
madini.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Balozi Noluthando
Malepe aliitaja Tanzania kama moja ya nchi bora zaidi kwa uwekezaji
kutokana na uwepo wa fursa nyingi za kibiashara huku akitaja uwepo wa
amani nchini Tanzania pamoja na ushirikiano wa kihistoria uliodumu kwa
muda mrefu baina ya Tanzania na Afrika Kusini kama nguzo muhimu katika
kufanikisha ustawi wa biashara baina ya mataifa hayo mawili.
“Hivyo
nawaomba sana muitumie vema fursa hii ya amani na ushirikiano tuliona
nao na wenzetu wa Tanzania kustawisha biashara zenu. Popote mnapohisi
kuna changamoto tunawakaribisha ofisi za ubalozi ili tuweze kujadili
namna bora ya kuzitatua huku pia tukijadili fursa nyingine zaidi,’’
aliomba Balozi Malepe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Bw Manish Thakrar
alisema pamoja na mambo mengine, nia ya jukwaa hilo ni kuunga mkono
jitihada za serikali katika kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nje ya
nchi kuja kuwekeza nchini Tanzania, huku akitaja suala la upatikanaji
wa huduma za kifedha za uhakika kama moja nguzzo muhimu katika
kufanikisha agenda hiyo.
“Hata hivyo Habari njema ni kwamba
ushirikiano wetu na benki ya NBC uliodumu kwa muda mrefu sasa umeendelea
kutuhakikishia upatikanaji wa huduma bora za kifedha. Tumefarijika
zaidi kusikia kwamba NBC wanaendelea kutuhamasisha kuhusu ushiriki wetu
kwenye soko la G-20 huku wakituhakikisha ufanisi zaidi kwenye
upatikanaji wa mitaji zaidi na huduma nyingine nyingi za kifedha,’’
alisema Bw Thakrar ambae pia lionyesha kuvutiwa zaidi na huduma ya
malipo ya mtandao ya NBC Connect.
No comments:
Post a Comment