JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Waziri Ulega ahamasisha wananchi kuingia sekta ya Mifugo na Uvuvi

Share This

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na waandishi habari katika  banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi   alipotembelea banda hilo kwenye  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisaini vitabu vya mabanda yaliyoshiriki  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Asema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amegungua mipaka ya neema kwa kila sekta

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema kuwa serikali imewekza katika sekta hiyo hivyo watanzania watumie fursa ya ufugaji na Uvuvi kutokana kuwepo kwa soko la uhakika.

Ulega aliyasema hayo kwenye la Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika viwanja vya  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ulega amesema kuwa sekta ya mifugo ya Uvuvi kuachana na biashara mazao yake kwa kula na kunywa ndio yanafanya kujenga afya.

Ulega amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imefungua mipaka hivyo kwa watanzania wanauhakika wa masoko ya ndani pamoja na masoko nje kuuza bidhaa zitotokanazo na Mifugo pamoja na Uvuvi.

Aidha amesema kuwa serikalo inatarajia kujenga miundombinu itayofanya ya kuvuta samaki ambayo mvuvi hana sababu ya kwenda mbali kutafuta samaki.

Ulega amesema kuwa ufugaji na Uvuvi kwa sasa unakwenda kisasa kutokana kuwepo watalaam ambao wanashauri na kuweza kufanya mtu kunufaika na kile anachofanya kwa kumpa faida zaidi ya mara mbili.

Waziri huyo amesema maonesho ya sabasaba wananchi wafike katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo watajifunza ufugaji na uvuvi wa kisasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad