JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Vipengele vya azimio la DP World havina tofauti na vipengele vya azimio la bomba la mafuta la Uganda na Tanzania

Share This

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Adv. Mohamed Salum,

VIPENGELE vya azimio la DP World havina tofauti na vipengele vya azimio la bomba la mafuta la Uganda na Tanzania lililopitishwa na Bunge mwaka 2017.

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Adv. Mohamed Salum, ameeleza kuwa azimio lililopitishwa na Bunge kuhusu DP World siyo jambo geni. Bunge lilipitisha azimio kuhusu bomba la mafuta kati ya Uganda na Tanzania mwaka 2017, lenye vipengele vinavyofanana kabisa na vipengele vya azimio la ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai kuhusu DP World.

Ameyasema hayo katika kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa kila siku kwenye televisheni ya UTV kutokea jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo anafafanua kuwa maswali yanayoulizwa sasa kuhusu kikomo cha mkataba, kugawana mapato na masuala mengine yatajadiliwa wakati wa kuandaa mkataba wa uwekezaji wa DP World nchini Tanzania, kwani hayamo kwenye azimio la Bunge.

Amesema kuwa sababu za mkataba huo kwenda bungeni ni kwa ajili ya kupata maoni ya wananchi ambayo hayafanywi na serikali kuu kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema katika mkataba huo hufanya michakato ya ndani na kusubiri ridhaa ya Baraza la Mawaziri na kisha  inakwenda bungeni kujadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad