JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MBUNGE WA JIMBO LA MBARALI (CCM) AFARIKI DUNIA

Share This

 

MAREHEMU FRANCIS LEONARD MTEGA

(01-06-1959 – 01-07-2023)

___________________

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Francis Leonard Mtega, Mbunge wa Jimbo la Mbarali (CCM) kilichotokea leo tarehe 01 Julai, 2023 kwa ajali ya kugongwa na Trekta (Power Tiller) shambani kwake Mbarali, Mkoani Mbeya.

 

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Francis Leonard Mtega. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wa Jimbo la Mbarali. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.

 

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

 

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.

 

Imetolewa na :           Kitengo cha Mawasiliano na Uhusianmo wa Kimataifa

                                                Ofisi ya Bunge

Dodoma

 

01 Julai 2023

 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad