JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MBUNGE VITI MAALUM KAGERA ATIMIZA AHADI ZAKE.

Share This


Na Abdullatif Yunus - Michuzi Blog Kagera.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Kagera Mh. Oliver Daniel Semuguruka amekabidhi ahadi yake ya Vifaa vya Ujenzi na Pesa Taslimu kwa Uongozi wa UWT Mkoa Kagera, ambayo aliahidi kipindi cha Baraza lililopita wakati akikabidhi Pikipiki Nane kwa Makatibu wa UWT Wilaya za Mkoa Kagera.

Ahadi hiyo ambayo ni Mifuko Thelathini ya Saruji, maalum kwa Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa Kagera, imekabidhiwa Rasmi kwa niaba yake na Ndg. Shafih Jumanne Rugomba Katibu wa Mbunge, ambaye amemuwakilisha katika katika Kikao cha Kawaida cha Baraza la UWT Mkoa Kagera, kilichofanyika mapema Julai 13, 2023 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera zilizopo Bukoba Manispaa.

Mifuko hiyo ya Saruji imepokelewa na Mwenyekiti wa UwT Mkoa Kagera Bi. Faidha Kainamula pamoja na Katibu wa UWT Mkoa Kagera Bi. Rebecca Magoma, sambamba na Kiasi cha  Shilingi Milioni Tatu laki mbili na nusu (3,250 ,000 ) ikiwa ni Mchango wa Vifaa vya Ujenzi Mchanga na Mawe na Nauli za Wajumbe wa Kikao hicho


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad