· Wimbi kuleta vionjo vipya kwa wapenzi wa tamthilia Tanzania
· Malkia Karen, Kinata MC, Chinno Kid rasmi ndani ya DStv na vibe kama lote!
Mambo
yanazidi kupamba moto ndani ya chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo
ndani ya DStv ambapo imezindua vipindi vyake vipya vya Wimbi sambamba
na Divas & Hustlers kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo mwezi huu
wa Julai. Vipindi hivi vya kuvutia vitapatikana kwenye chaneli ya Maisha
Magic Bongo, DStv CH. (160). Uzinduzi huu unathibitisha jitihada za
DStv katika kuwapa wateja wetu chaguo bora la vipindi na huduma ya
televisheni kwa gharama nafuu.
Akizungumza katika hafla ya
kuzindua vipindi hivyo vipya vya chaneli ya Maisha Magic Bongo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Bi. Jacqueline
Woiso amesema kuwa "Tunafurahi kuwatambulisha watazamaji wetu vipindi
vipya vya kusisimua vya 'Wimbi' na 'Divas and Hustlers. Kuingizwa kwa
vipindi hivi vipya ndani ya DStv kumezingatia sana maoni ya watazamaji
na tunaamini kuwa watavifurahia sana.
Wimbi" ni tamthilia ya Kitanzania inayolenga visa vya mapenzi, tamaa, mali, na siri za familia. Tamthilia hii itakuwa inarushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 4:00 usiku, kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo, DStv Ch. (160).
Tamthilia
hii pia itakuwa na wasanii maarufu na wakongwe akiwemo Blandina
Chagula maarufu kama Johari, Natasha Ma Mvi, na Yusuph Mlela na wengine
wengi. "Wimbi" ilianza kuonekana hewani tarehe 3 Julai 2023, na
tunaiimani itawavutia wapenzi wa tamthilia kwa hadithi yake ya
kusisimua na uigizaji bora.
Aidha, "Divas and Hustlers" itaanza
kurushwa siku ya Alhamisi, tarehe 13 Julai 2023, na itapatikana pia
katika chaneli ya Maisha Magic Bongo, DStv Ch. (160), kila Alhamisi saa
3:00 usiku.
Kipindi
hiki kinashirikisha mastaa maarufu kama vile Chinno kid mcheza mziki
maarufu, mwanamuziki Malkia Karen, mkali wa singeli Kinata MC, Rey
Jones, na wengine wengi. "Divas and Hustlers" imejipanga kuleta
Mapinduzi ya burudani kupitia watu hawa mashuhuri katika tasnia ya
burudani hapa nchini.
Kama haitoshi, wateja wa DStv wataendelea
kufurahia vipindi vingine kama vile "Jua Kali," inayoruka kila siku ya
Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku, tamthilia ya "HUBA" Jumatatu
hadi Ijumaa saa 3:00 usiku,tamthilia ya "Pazia" Jumatatu hadi Jumatano
saa 1:30 usiku, na vichekesho vya "Kitimtim" Jumatatu na Jumanne saa
3:00 usiku.
Aidha,
wapenzi wa vichekesho wataendelea kuongeza siku za kuishi kupitia
vichekesho vya "Return of Original Comedy" kila Jumapili saa 3:00 usiku
na "Watubaki " kila Jumamosi saa 3:00 usiku ndani ya Maisha Magic Poa,
DStv Ch. (144), inayopatikana kwenye kifurushi cha DStv Poa
kinachopatikana kwa Tshs. 10,000/-
Wapenzi
wa soka nao hatujawaacha nyuma, kupitia chaneli zetu za SuperSport, pia
tumejipanga kuleta burudani ya moja kwa moja katika msimu mpya wa soka
utakaoanza rasmi Agosti 11 mwaka hu, kwa mfumo wa picha anagvu yaani
HD, kwa wateja wetu wakubwa wa DStv. Mashabiki wa soka nchini Tanzania
wanapaswa kukaa mkao wa kula, DStv kupitia SuperSport itaonyesha mechi
zote 380 za Ligi Kuu kwenye chaneli yetu maalum ya SuperSport Premier
League Ch. (223) na kuwapa uhuru wa kuchagua kutazama mechi hizo kwa
lugha adhimu ya Kiswahili.
Hii
haiishi hapa, kupitia SuperSport pia tumejiandaa kuonyesha zaidi ya
mechi 300 za kusisimua kutoka La Liga kwenye chaneli yetu ya SuperSport
La Liga Ch. (224), pamoja na mechi zaidi ya 300 za kusisimua kutoka
katika ligi ya Serie A.
Amewataka
wale wote ambao hawajajiunga na DStv kufanya hima kuwahi ofa maalum
iliyopo sokoni kwa sasa ambapo mteja hupata seti kamili ya DStv kwa
shiling 99,000 tu! Amesema hii ni ofa ya muda maalum hivyo ni vyema
wakaichangamkia ili wasipitwe na moto wa burudani unaoendelea kuwaka
ndania ya DStv.
Kulipia kifurushi cha DStv bonyeza *150*53# au piga 0659 070707 kujiunga na DStv!
No comments:
Post a Comment