JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MRADI WA FEEL FREE WATANGAZA MAWAZO YA KIBUNIFU 08 YATAKAYONUFAIKA NA MFUKO WA  UBALOZI WA USWISSI NA NORWAY 

Share This

 

Na Khadija Seif, Michuziblog
NAFASI Art Space imetangaza vikundi nane vya sanaa vilivyoshinda mawazo ya kibunifu kupitia mradi wa Feel Free na kushinda jumla ya sh milioni 187,260,000 chini ya ufadhili wa ubalozi wa Uswissi na Norway.

Akizungumza na Wanahabari Leo 06,2023 Jijini Dar es salaam akitangaza vikundi hivyo Mwenyekiti wa Bodi Nafasi Art Space Paul Ndunguru ameeleza hii ni mara ya tatu toka programu hiyo imeanza ambapo walioshinda ni wale walioandika wazo la kibunifu la upekee.

Hata hivyo programu hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuwatia moyo wasanii, wadau wa Sanaa, taasisi zinazojihusisha na ubunifu na sanaa, walitakiwa kupeleka wazo la kibunifu wanaloweza kufanyika kazi kisha kupewa fedha za kuendesha miradi husika kwa uhuru.

"Zaidi ya watu na vikundi 100 vilijitokeza kuleta mawazo yao, lakini hivi vinane vilishinda na sasa vitakwenda kutekeleza kile walichokiomba katika miradi yao,"alisema na kuongeza kuwa kuna program nyingi kwenye taasisi hiyo wasanii waendelee kuzifuatilia ili wanufaike.

Aidha ametaja vikundi vilivyonufaika na mradi wa ''Feel Free "kuwa ni Fahari Yetu kutoka Iringa, Adea Tanzania kutoka Mtwara, Victoria Alex John kutoka Tanga, Wifi women prints kutoka Zanzibar, Emedo kutoka Mwanza na Refixit kutoka Dar es Salaam.

Vingine ni Scolastica Sultan na mradi wa ndoto ya Kalista na bendi ya muziki ya Bahati wote hawa wakitoka Dar es Salaam.

Miongoni mwa wanufaika hao Scolastica Sultan alisema mradi wake umelenga kuwasaidia wanawake wanaolea watoto bila ya baba (Single mother) kuwaelimisha namna ya kuinuka baada ya kubaini wapo waliopoteza mwelekeo baada ya kupata ujauzito wakiwa wadogo.

Naye Aliabu Sadock kutoka Taasisi ya Fahari Iringa ameongeza kuwa wao watakusanya taarifa za masimulizi yaliyopita ya kikoloni kutoka mkoani humo na kuyarudisha kwa jamii kwa ajili ya kujifunza maadili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad