Mwanamuziki Luizer Mbutu Nyoni ameweka historia usiku wa Jumatano Mei 11, mwaka huu kwa kuwa mwanamke wa kwanza nchi kushinda nafasi ya Mwenyekiti Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika ukumbi wa Dar Modern ulioko Magomeni Mikumi mtaa wa Ifunda jijini Dar es Salaam.
Luizer mwimbaji tegemeo na wa siku nyingi wa Twanga Pepeta, aliwashinda kwa mbali wapinzani wake Mwinjuma Muumini (Aliyeshika nafasi ya pili) na Said Kaunga.
Mwimbaji wa Sikinde, Abdallah Hemba akafanikiwa kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyokuwa akiipigania na mwanamuziki wa Tabora Jazz, Ramadhani Kitenge.
Katika nafasi ya Katibu Mkuu meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti alimbwaga Hassan Msumari aliyekuwa akitetea kiti chake.
Katibu Msaidizi wa Chamudata aliibuka wakili Msomi Baraka Elias Sulus ambaye alikuwa mgombea pekee na hivyo kura za ndio zikampitisha kwa kishindo, japo yeye mwenyewe hakuwepo ukumbini.
Nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji zilizokuwa na mchuano mkali, zikaenda kwa Profesa Abuu Omar, Cecy Jeremiah Logome Mwasi Kitoko, Bernedict Berno Sanga, Said Mdoe, Gabriel Bakilana na Rhobi Chacha. Wagombea wengine Matei Joseph, Shomary Ally, Tabu Mambosasa, Andrew Mwampashi na Sholinda Mwezimpya kura hazikutosha.
Uchaguzi wa Chamudata ulifanyika kwa uwazi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Kamanda Mstaafu Jamal Rwambo (SACP) na kufanya zoezi hilo likamilike bila malalamiko ya upande wowote.
Hiyo ilijidhihirisha pale wagombea walioshindwa wote walipojitokeza meza kuu na kutia Saini fomu za matokeo na walipopewa nafasi ya kusema machache baada ya uchaguzi walikubali matokeo na kupongeza mchakato mzima wa uchaguzi huo ulivyofanyika.
SAFU MPYA YA UNGOZI WA CHAMUDATA NI HII HAPA:
MWENYEKITI
Luizer Morris Nyoni
MAKAMU MWENYEKITI
Abdallah Hamis Hemba
KATIBU MKUU
Said Nassoro Kibiriti
KATIBU MSAIDIZI
Baraka Elias Sulus (Advocate)
WAJUMBE (NAFASI SITA):
1. Abbu Omar Abubakar
2. Cecy Jeremiah Lugome
3. Said Abdillahi Mdoe
4. Bernedict Berno Sanga
5. Gabriel Byabato Bakilana
6. Rhobi Abubakari Chacha
Nafasi za Mweka Hazina na msaidizi wake hazikujazwa kwa kuwa hakuna aliyejitokeza kugombea. Hivyo mwCHAMUDATA MPYA YAPATIKANA ...Luizer kidedea, Msumari aanguka
Luizer (Mbutu) Nyoni amefanikiwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano jijini Dar es Salaam.
Katika uchaguzi huo wa Chamudata uliofanyika kwenye ukumbi wa Dar Modern ulioko Magomeni Mikumi, Luizer mwimbaji tegemeo wa Twanga Pepeta, aliwashinda kwa mbali wapinzani wake Mwinjuma Muumini (Aliyeshika nafasi ya pili) na Said Kaunga.
Mwimbaji wa Sikinde, Abdallah Hemba akafanikiwa kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyokuwa akiipigania na mwanamuziki wa Tabora Jazz, Ramadhani Kitenge.
Katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Chamudata, meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti akambwaga Hassan Msumari aliyekuwa akitetea kiti chake.
Katibu Msaidizi wa Chamudata ni Wakili Msomi Baraka Elias Sulus ambaye alikuwa mgombea pekee na hivyo kura za ndio zikampitisha kwa kishindo.
Nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambazo zilikuwa na mchuano mkali, zikaenda kwa Abuu Omar, Cecy Jeremiah Logome, Bernedict Berno Sanga, Said Mdoe, Gabriel Bakilana na Rhobi Chacha huku kura zikishindwa kutosha kwa Matei Joseph, Shomary Ally, Tabu Mambosasa, Andrew Mwampashi na Sholinda Mwezimpya.
Uchaguzi wa Chamudata ulifanyika kwa uwazi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Kamanda Mstaafu Jamal Rwambo (SACP) na kufanya zoezi hilo likamilike bila malalamiko ya upande wowote.
Hiyo ilijidhihirisha pale wagombea walioshindwa walipopewa nafasi ya kusema machache baada ya uchaguzi ambapo wote walikubali matokeo na kupongeza mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika.
SAFU MPYA YA UNGOZI WA CHAMUDATA NI HII HAPA:
MWENYEKITI
Luizer Morris Nyoni
MAKAMU MWENYEKITI
Abdallah Hamis Hemba
KATIBU MKUU
Said Nassoro Kibiriti
KATIBU MSAIDIZI
Baraka Elias Sulus (Advocate)
WAJUMBE (NAFASI SITA):
1. Abbu Omar Abubabar
2. Cecy Jeremiah Lugome
3. Said Abdillahi Mdoe
4. Bernedict Berno Sanga
5. Gabriel Byabato Bakilana
6. Rhobi Abubakari Chacha
Nafasi za Mweka Hazina na msaidizi wake hazikuweza kujazwa kwa kuwa hakuna aliyejitokeza kugombea. Hivyo Mwenyekiti wa uchaguzi akatangaza kwamba zitajazwa siku za usoni kwa kufuata muongozo wa katiba ya Chamudata.
Uchaguzi wa Chamudata ulifanyika kwa uwazi wa hali ya juu chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Kamanda Mstaafu Jamal Rwambo (SACP)
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Kamanda Mstaafu Jamal Rwambo (SACP) akiwa meza kuu na wasimamizi

No comments:
Post a Comment